Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Babylus Mashauri (kushoto) akipeana mkono na Meneja wa benki ya Taifa ya Baishara (NBC) tawi la Bukoba, Mathias Muhangirwa baada ya benki huyo kukabidhi jumla ya tani nne za saruji kwaajili ya ujenzi wa shule ya msingi Ibosa. 

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Babylus Mashauri (kushoto) akipokea jumla ya tani nne za saruji kutoka kwa Meneja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) tawi la Bukoba, Mathias Muhangirwa baada ya benki hiyo kuchagia saruji kwaajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Ibosa.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Babylus Mashauri (Kulia) akikabidhi jumla ya mifuko 80 ya saruji iliyotolewa na  Benki ya NBC kwa kamati ya ujenzi ya shule ya msingi Ibosa.

 

Katika kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira bora, benki ya taifa ya biashara (NBC) imechangia tani nne za saruji kwaajili ya kufanikisa ujenzi wa madarasa matano ya shule ya msingi Ibosa iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Kagera.

 Msaada huo ni sehemu ya urudishaji kwa jamii ambapo utsaidia kufanya maboresho ya miundombinu ya madarasa na hatimaye kupunguza msongamano wa wanafunzi unaoikabili shule hiyo hivi sasa.

 Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa NBC tawi la Bukoba, Mathias Muhangirwa alisema mchango huo utasaidia katika kuboresha miundombinu yamadarasa ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira bora.

Aidha Mathiasi alisema ili mpango wa serikali wa utoaji elimu bure ufanikiwe ni lazima wadau mbali mbali wajitokeze kuchangia katika ujenzi wa miundombinu kama madarasa lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya wanafunzi wanaojitokeza kuanza darasa la kwanza kila mwaka.

 “Kama sehemu ya urudishaji kwa jamii tumeona ni vema kuunga mkono jitihada hizi za uboreshaji wa miundombinu kwa kutoa tani nne za saruji ambazo tunaamini zitasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani” alisema Meneja huyo.

Akipokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Babylus Mashauri alisema kwa sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 789 ambapo kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya elimu shule hiyo ilibidi iwe na maddarasa 14 hata hivyo mpaka sasa ina madarasa tisa.  

“Tuna upungufu wa vyumba vitano Kwahiyo unaweza kuona jinsi kulivyo na msongamano kwenye madarasa hayoo, kwa msaada huu utakuwa ni chachu ili tuweze kuongeza vyumba ili kukidhi mahitaji ya shule hii,” alisema.

Share To:

Post A Comment: