MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika kwenye ofisi za Tarura wilaya ya Tanga wakati wa ziara yake
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akilakiwa  meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene mara baada ya kufika kwenye ofisi za Tarura wilaya ya Tanga wakati wa ziara yake

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akisistiza jambo kwa Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene kushoto wakati wa ziara yake
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akionyeshwa maeneo mbalimbali kwenye mifereji wakati wa ziara yake na Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akionyeshwa maeneo mbalimbali kwenye mifereji wakati wa ziara yake na Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wa pili kutoka kulia akitembelea  maeneo mbalimbali wakati wa ziara yake wa kwanza kushoto ni Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wa pili kutoka kushoto  akionyeshwa maeneo mbalimbali kwenye mifereji wakati wa ziara yake na Diwani wa Kata ya Msambweni (CCM) Godias Kimath na kwanza kulia Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Mh  Ummy Mwalimu ameanza kazi rasmi leo  za jimbo kwa kutembelea ujenzi na kukagua miradi ya barabara, mifereji na madaraja ya kata nne ambazo ni Mnyanjani, Mabawa, Msambweni na Ngamiani kati za halmashauri ya Jiji la Tanga ambazo zitagharimu kiasi cha sh.bilioni 2.9.

Ummy alisema kuwa ameanza kazi kwani Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliahidi na sasa  kinatekeleza Ilani ikiwemo matengenezo ya barabara ya karume mpaka  machinjioni mita 600 ambayo itajengwa kwa kiwango cha changarawe, barabara ya karume mpaka zahanati ya kwanjeka kwa kiwango cha changarawe,
 
Huku akiitaja pia barabara ya 11 na 12 kuzunguka soko la Ngamiani  itawekwa lami,barabara ya Mabawa mpaka Msambweni ambayo itaongezwa lami yenye urefu wa kilometa 2.

Aidha pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia fedha Tarura ambazo zitaenda kuboresha miundo mbinu ya barabara ndani ya Jimbo la Tanga Mjini na kuwa kazi ndiyo zimeanza na hatakuwa mbunge wa ofisini bali muda mwingi atakuwa ni wa kutembelea miradi na kutatua kero za wananchi wa Tanga.

Naye Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene amesema kuwa  kwa mwaka huu wa fedha wamesaini mikataba mitano  ambapo ndani ya siku 14 wataanza kazi utekelezaji .
 
Miradi hiyo ipo itayayotekelezwa kwa kiwango cha changarawe, lami ,ujenzi madaraja na ukarabati wa mifereji  ndani ya Jiji la Tanga barabara na amesema kuwa watendelea kufanya kazi kama azma ya serikali ya hapa kazi tu.

kwa upande wa madiwani  akiwemo Yakub Nuru ambaye  Diwani wa Mnyanjani wametoa shukrani kwa mh. Ummy Mwalimu pamoja na serikali kupitia Rais Magufuli  kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya barabara. 
 
Awali naye Diwani wa Kata ya Mabawa, Athumani Babu alisema kuwa ilani ya chama cha mapinduzi imeanza kutekelezwa  kwani barabara ya kutoka komesho mpaka  chai bora yenye km 1   imeweka lami .
 
Hata hivyo kwa upande wake Diwani wa kata ya Ngamiani Kati, Habibu Mpa ametoa shukrani zake kwa mh. mbunge ummy mwalimu kwa  kufuatilia ahadi ya waziri mkuu wakati akifungua kampeni  za Mbunge kuhusu kuweka lami barabara ya 11 na 12 yenye urefu wa mita 600.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: