Monday, 12 October 2020

WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZILIZOPO VYAMA VYA USHIRIKA ILI KUONDOKANA KUWA TEGEMEZINA NAMNYAK KIVUYO,  ARUSHA

Wanawake wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika vyama ushirika ikiwemo nafasi uongozi ili kujiendeleza kiuchumi nakuleta maendeleo kwa jamii nakuondokana na umaskini pamoja na utegemezi.


Akizungumza katika kongamano la wanawake wa vyama vya ushirika,akiba na mikopo(Saccos) lililofanyikia jijini Arusha ,Naibu Mrajis wa vyama vya ushirika wa tume ya maendeleo nchini Tanzania,Charles Malunde alisema ingawa ushirika unazidi kushamiri katika sekta mbalimbali za kiuchumi na vyama kujiendesha kwa kufuata misingi ya kimataifa bado kuchangamoto katika masuala ya jinsia  na nafasi ya mwanamke katika uongozi.


“Ushiriki wa wanawake katika sekta ya ushirika umekuwa kidogo sana hivyo hali hii ikiendelea kuwa hivi itapelekea kutokuwa na uendelevu  katika shughuli za kiushirika  katika miaka ijayo na kukosekana  kwa chombo cha kitaifa  cha kuwaunganisha  wanawake katika sekta ya ushirika  kunapelekea kukosa uwakilishi katika anga za kimataifa  na kukosa fursa za maendeleo zilizoelekezwa  katika makundi haya,”alisema Naibu Mrajis.

Malunde alisema ushiriki mdogo wa wanawake katika vyama ushirika nchini kunapelekea changamoto katika jamii zinzozunguka vyama vya ushirika kutokuwa na usawa wa kijinsia kuhofia kugombea nafasi za uongozi na kushindwa kushiriki kikamilifu katika maamuzi pamoja na kutokuwa na chombo cha kitaifa cha kuwaunganisha wanawake waliokatika ushirika wa akiba na mikopo.


Alifafanua kuwa kulingana na sensa ya mwaka 2012 wanawake walikuwa ni asilimia 51.3 ya idadi ya watu wote hapa nchini ambapo kwa upande wa nguvu kazi walikuwa asilimia 53.3 ,wanaojihusisha  na biashara ndogo ndogo na za kati asilimia 54 lakini pamoja na takwimu hizo idadi ya wanawake wanaozifikia huduma za kifedha ilibaki kuwa ni asilimia 60 huku wanaume ikiwa ni asilimia 70.

“Kutokana na takwimu hizo utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali katika kuweza kupata huduma za kifedha ikiwemo mikopo kwa kukosa dhamana riba kuwa kubwa pamoja na masharti magumu ya mikopo lakini kupitia kongamano hili mnaweza kuona pia mwanamke hajiamini na ndio maana fursa nyingi zinampita pembeni,”alisema.

Aidha alisema kuwa kutokana na jukwaa hilo serikali inamatarajio kuwa wanawake waliopo katika saccos watakuwa ni chachu ya maendeleo ya ushirika wa akiba na mikopo kwa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi a vyama,kuhamasisha uwekeji wa akiba kwa malengo na urejeshaji wa mikopo kwa muda ,shughuli za kujiongezea maarifa pamoja na kushiriki kuiwakilisha nchi katika mikutano ya kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake makamo mwenyekiti wa muungano wa vyama hivyo,Somoe I smail alisema wanawake ni kundi muhimu katka kuleta maendeleo chanya kwenye jamii hivyo wachangamkie fursa za kujiunga katika vyama vya ushirika kwani vyama hivyo vinaenda chini hadi kwenye ngazi ya jamii ambazo bado hazijafikiwa na taasisi za fedha.

“wanawake tunaweza kufanya shughuli za maendeleo na kuwa viongozi hivyo tusisubiri wanaume wafanye kazi peke yao na kutunza familia kwani ili familia iweze kuendelea inahitaji nguvu mbili yaani baba afanye kazi na mama pia na kwa kufnya hivyo tutaweza kutunza familia zetu na kutumiza wajibu wetu kwa jamii na Taifa kwa ujmla,”alisema Ismail. Nao baadhi ya washiriki kutoka Arusha Maria Maembe alieleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili wanawake ni kutojiamini hali inayowafanya washindwe kuchangamkia fursa mbalimbali katika jamii ambapo wakipata ujasiri wanaweza kufanya kitu kenye jamii na wakafanikiwa na kutolea mfano taasisi nyingi zinazoongozwa na wanawake kuwa na tabia ya kufanya vizuri.Naye Goleth Bosco kutoka mkoa wa Kagera  alisema kupitia jukwaa hilo wataweza kujenga na kusaidiana kuingia katika uongozi na kupambana na changamoto zinazowakabili kwani mwamko wa wanawake bado ni mdogo katika jamii.


MWISHO

No comments:

Post a comment