Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akiongea na wanawake wa tarafa ya Pawaga wakati wakiweka mikakati ya kupata kura nyingi za wagombea wa CCM wote
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Nicolina Lulandala akisisitiza jambo wakati wa kuomba kuwaomba wanawake wa UWT tarafa ya Pawaga kwa ajili ya kuzitafuta kura za wagombea wa chama cha mapinduzi
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Nocolina Lulandala akisisitiza jambo wakati wa kuomba kuwaomba wanawake wa UWT tarafa ya Pawaga kwa ajili ya kuzitafuta kura za wagombea wa chama cha mapinduzi

Na Fredy Mgunda,Pawaga.

UMOJA wa wanawake Mkoa wa  Iringa (UWT) wameeendelea kuzitafuta kura za chama cha mapinduzi (CCM) kata kwa kata kwa lengo la kuhakikisha wanapata kura nyingi za mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli,madiwani na wabunge ili chama hicho kiendelee kushika dola.
Akizungumza kwenye mkutano wa wananwake wa tarafa ya Pawaga mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Nicolina Lulandala aliwaomba wanawake wote wa tafara hiyo kuhakikisha wanazitafuta kura nyingi za wagombea wa chama cha mapinduzi ili wawee kushinda kwa kishindo.

Alisema kuwa Rais Dr Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa elimu bure,kukarabati majengo ya shule na kujenga majengo mapya mengi na amefuta michango shuleni hivyo wanawake wa Iringa wanapaswa kumtafutia kura Dr John pombe Magufuli.

Lulandala aliongezea kwa kusema kuwa katika sekta ya elimu wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wanapana mikopo kwa wakati na ndio maana kwa kipindi cha miaka mitano hakuna maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ilivyokuwa miaka ya huko nyuma.
Lulandala aliwaomba wanawake wa mkoa wa Iringa kutumia ushawishi wao kuhakikisha wanampigia kura nyingi mgombea huyo wa chama cha mapinduzi Dr John pombe Magufuli kwa kuwa anauwezo wa kuliongoza taifa hili kimaendeleo kuliko wagombea wengine.

Alisema kuwa umoja wa wanawake Mkoa wa  Iringa (UWT) unafanya ziara katika tarafa zote mkoa wa Iringa ili kuhakikisha wanawake wa mkoa wa Iringa wanakwenda kuzitafuta kura za chama cha mapinduzi (CCM) kuanzia udiwani,ubunge hadi urais hivyo wanawake waliohudhulia kongamano hilo lilikuwa na lengo la kuhakikisha CCM inapata kura za kutosha kuliko vyama vingine.


Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Nocolina Lulandalai alisema kuwa chama cha mapinduzi Iringa vijijini kimejipanga kuhakikisha kinaleta maendeleo katika kata ya tarafa ya Pawaga kwa kuwa tayari wamejipanga kwa mikakati imara ya kufanya kazi za kimaendeleo.

 “Najua kina mama wanajua kukiwa na tatizo kiafya hakuna shughuli za kimaendeleo ambazo zitafanyika kwa urahisi hivyo tupeni miaka mitano hii tuboreshe sekta ya afya kwa kuwa viongozi wa CCM wamejipanga kutatua tatizo hilo kama ambavyo tayari tumejenga hospitali ya wilaya hapa Pawaga na tunaendelea kuboresha vituo vya afya”alisema Hongoli

Aidha Hongoli alisema kuwa tatizo la maji kwenye baadhi ya vijiji na vijiji vingine tatizo hilo limetatuliwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufulu kwa ushirikiano na mbunge wa jimbo la Isimani William Lukuvi.

Alisema kuwa wananchi wa tarafa ya Pawaga wanategemea kilimo kwa kiasi kikubwa hivyo ni lazima kuwasaidia kupandisha thamani ya mazao ili wakulima hao wapate faida ya kilimo hicho.

Naye Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele ambaye alikuwa mgeni aliwaomba wanawake wa tarafa ya Pawaga kuhakikisha wanazitafuta kura za wagombea wanaotokana na chama cha mapinduzi (CCM) ili kuhakikisha maendeleo ya Tarafa hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano wa mkutano wa wanawake wa Tarafa ya Pawaga, Mtewele alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwachagua wagombea wa chama cha mapinduzi kwa kuwa chama hicho ndio kinaweza kuleta maendeleo tofauti na vyama vingine
Alisema kuwa chama cha mapinduzi kimejipanga kuhakikisha kinaleta maendeleo katika tarafa ya Pawaga kwa kuwa tayari wamejipanga kwa mikakati imara ya kufanya kazi za kimaendeleo.
Aidha Mtewele alisema kuwa tatizo la maji limetatuliwa katika kata hizo kutokana kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufulu.
Alisema kuwa wananchi tarafa ya Pawaga wanategemea kilimo kwa kiasi kubwa hivyo ni lazima kuwasaidia kupandisha thamani ya mazao ili wakulima hao wapate faida ya kilimo hicho.
Mtewele alimazia kwa kuwaomba wanawake wa Pawaga kumchagua mgombea udiwani,ubunge na mgombea urais wa CCM kwa kuwa hao ndio wanaweza kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa kata hizo.
 .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: