Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza na wananchi wa Kata ya Mzingani Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimnadi mgombe udiwani Kata ya Mzingani Jijini Tanga Abdurhamani Shiloo juzi wakati wa mkutano wake wa kampeni
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akimuombe kura Mgombe Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga(CCM) Ummy Mwalimu
Sehemu ya Umati wa Wakazi wa Kata ya Mzingani Jijini Tanga wakimsikiliza kwa umakini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Sehemu ya Umati wa Wakazi wa Kata ya Mzingani Jijini Tanga wakimsikiliza kwa umakini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Sehemu ya Umati wa Wakazi wa Kata ya Mzingani Jijini Tanga wakimsikiliza kwa umakini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Msanii Mchina Mweusi akitumbuiza wakati wa mkutano huo
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo wa kampeni
***

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ametangaza neema kwa wavuvi kwenye Jiji la Tanga baada ya kuwahaidi kwamba watawezeshwa kupata mikopo nafuu na zana za kisasa za uvuvi ili waweze kunufaika kupitia sekta hiyo na hatimaye kujikwamua kiuchumi.

 

Sambamba na hilo ameahidi pia kuipatia ufumbuzi changamoto ya barabara ya kwenda Machinjioni –Msikitini ili kuhakikisha inakuwa kwenye kiwango kizuri kuliko ilivyokuwa sasa.

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika Dunia Hotel Kata ya Mzingani Jijini Tanga uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.

Alisema kwamba suala la wavuvi atalishughukia kwa kuhakikisha changamoto ambazo wanakabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao anazipatia ufumbuzi ili kuwawezesha kufanya shughuli hizo bila vikwazo.

Ummy alisema pia atahakiksha anawezesha mazingira ya uwepo wa barabara ya Mzingani hadi Machinjioni kwa kupasua barabara ya mtaa wa msikitini ili kuwawezesha wananchi kuitumia kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali.

“Kuhusu suala la taa za barabara nitalifanyia kazi kuhakikisha mitaa yote muhimu kwenye kata ya Mzingani inawaka nyakati za usiku kuweza kulinda usalama wa watoto hivyo ninawaomba wananchi wa Mzingati mnichague kwani nina mipango mingi ya kimaendeleo lakini pia Oktoba 28 mchagueni kwa kuwa nyingi za kishindo Rais Dkt John Magufuli“,alisema.

Hata hivyo alisema katika kipindi cha Miaka mitano iliyopita Serikali  ya CCM ilijielekeza katika kujenga Miundombinu ya Hospitali, Zahanati na Vituo Afya  na kuwa katika miaka mitano ijayo CCM itajielekeza ktk kuhakikisha maboresho ya bima ya Afya ili watu wengi waweze kupata huduma za Afya bila vikwazo.

Sambamba na hilo Ummy alieleza kuhusu  suala la  CT Scan  ambapo aliwaambia wana Mzingani kwamba kuna maneno yanaelezwa kwamba alichukua CT Scan Mashine ya Bombo na kuipeleka Hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam.

“Labda niwaambieni wapuuzeni maana wameanza kupagawa kwanza sisi hatukuwa na hiyo  mashine ila kuna mdau alitaka kutusaidia ikabidi tutafute fedha za kujenga Jengo kwa ajili ya kuiweka mashine hiyo ambayo  itasaidia sana kupunguza safari za kwenda Kilimanjaro na tayari fedha zimeshapatikana”Amesema Ummy Mwalimu.

Share To:

Post A Comment: