Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi (kushoto) akimkabidhi juzi Mwalimu Mstaafu kutoka Wilaya ya Singida  Amosi Njoghomi kiasi cha shilingi milioni 18.8 zilizookolewa kutoka kwa mmoja wa wakopeshaji wa ‘Riba Umiza.’ Mwalimu Njoghomi alikopa shilingi milioni 2, lakini mkopeshaji alimtaka arejeshe fedha taslimu shilingi milioni 31 hadi serikali ilipoingilia kati na kumsaidia.

 

Na Edina Alex, Singida 


TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imeokoa sh.milioni 33.5 walizokopeshwa watumishi wa umma wastaafu na makampuni ya kukopesha fedha zenye riba kubwa maarufu kama mikopo umiza bila ya kufuata sheria.

Akitoa taarifa ya utekelezaji huo juzi  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida,  Adili Elinipenda  alisema operesheni hiyo wameifanya kufuatia agizo la mkuu wa mkoa huo la kuwatokomeza wakopeshaji haramu  ambao wamekuwa wanawakandamiza  wananchi  hasa watumishi wa umma  wanao karibia kustaafu.         

  "Mheshimiwa mkuu wa mkoa  Takukuru mkoani hapa tumejipanga kikamilifu kuhakikisha hawa wakopeshaji umiza  tunawamaliza kabisa  ndani ya mkoa wa Singida  na kwa kukuhakikishia leo  utawakabidhi wahanga kiasi cha sh.  mil 33.5  zilizotoka kwa wakopeshaji haramu. "alisema Elinipenda.

 Aidha Elinipenda aliyataja makampuni hayo  yaliyorudisha fedha za wananchi na watumishi wa umma kuwa ni kampuni ya Bomang Microfinance ya Singida mjini ambayo ilimkopesha Mwalimu Mstaafu Albert Sungi  Mpashi kiasi Cha shilingi 7,200,000  na kumtaka arejeshe shilingi 17,000,000  huku million 18,800,000 zimeokolewa  kutoka kwa mkopeshaji  Biseko Mungeta Kazungu  wa Singida mjini  nae alimkopesha Mwalimu Mstaafu  kiasi Cha shilingi Mlion 2,000,000 na kumtaka arejeshe  shilingi Milioni 31,000,000.

Wengini ni kampuni ya Magirei Company Lmt (Micro Credit) ya Singida mjini imerejesha fedha  za  Garase Kajuna  shilingi  17,000,000 , Huku Widop Company Ltd.

ikirejesha  shilingi  2400,000 kwa bi Lucia Petro Nyika Muuguzi Mstaafu   huku wengine ni Angelva Financial Lmt na Mwita Creditors ya Manyoni.

 Kwa upande wao  wahanga hao Albert Sungi ,  Garase Kajuna na bi  Lucia Nyika  walimshukuru Raisi Mgufuli  na uongozi wa Serikali ya awamu ya tano kwa kuwakumbuka wanyonge   maana baadhi yao walisha poteza matumaini ya kuishi kama watumishi wastaafu'

 "Tunamshukuru  Rais wetu Magufuli hakika Mungu ametuletea nabii sio tu Rais kwani  kwetu amekuwa baba wa wanyonge  tulipoteza matumaini kabisa lakini kwa uongozi wake makini tunacheka na kutabasamu" alisema mmoja wa wahanga hao.

Aidha wamewashauri  watumishi wengine ambao bado wapo katika utumishi  kujiandaa vuzuri ili wanapo achana na utumishi wasijiingize kwenye mikopo hiyo maana wakopeshaji hao haramu au umiza wanawatamani wastaafu au waliokwisha kustaafu.

Akikabidhi fedha hizo kwa  wahanga hao  Mkuu wa Mkoa wa Singida,  Dk. Rehema Nchimbi  aliwapa pole na kuwahakikishia  kuwa wakopeshaji haramu  ndani ya mkoa huo lazima wabadilike na kufanya kazi zingine  huku akiwapongeza watumishi wa TAKUKURU kwa utekelezaji kazi hiyo.           

"Mbadilike nyie wakopeshaji umiza  hivi hamuogopi Mungu alichokopa mtu na anachorejesha mbona haviringani lazima tuwatokomeze hii sio Serikali ya mchezo mchezo ." alisema Nchimbi.

Share To:

Post A Comment: