Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akizungumza wakati wa kufunga Kongamano la Nne la Mwaka la TEHAMA,jijini Dar es Salaam.


KatibuMkuuwaWizarayaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano(SektayaMawasiliano) Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw Emmanuel Tutuba (wa pili kushoto) na Naibu KatibuMkuu (Mawasiliano) Dkt Jim Yonaz(wa tatu kushoto) akisalimiananaDkt. Godwill Wanda, Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara Taifa, Baada ya Kongamano la Nne la Mwaka la TEHAMA kufungwarasmi.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu waWizara hiyo Dkt. Jim Yonaz baada ya kufunga Kongamano la Nne la Mwaka la TEHAMA, jijini Dar es Salaam.

 

 





Na Faraja Mpina - WUUM, Dar es Salaam

 

Katibu MkuuwaWizarayaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano (SektayaMawasiliano) Dkt. Zainab Chaula ameiasa jamii ya kitanzania kutumia simu janja kutafutia fursa mbalimbali za kujitafutia kipato ili kuinua uchumi binafsi na nchi kwa ujumla.

 

Dkt. Chaulaa lizungumza hayo alipokuwa akifunga Kongamano la Nne la Mwaka la TEHAMA lililofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 7 hadiOktoba 9, 2020.

 

“Tuzitumie simu janja vizuri kwa kutafuta fursa za kutuinuakiuchumi, tusitumie simu hizo kuperuzi kwa ajili ya burudani pekee bali tufunguke tutafute fursa za kiuchumi kwakutumia simujanja zilizounganishwa na mtandao ili maendeleo yapatikane kwa mtu mmoja mmoja naTaifa kwa ujumla”, alizungumzaDktChaula

 

DktChaula ametoa rai kwa wadau kutoka taasisi za umma nabinafsi walioshiriki katika Kongamano hilo kutekeleza yale yaliyo ndani ya uwezo wao, wasiiachie Serika ifanye kila kitu kwa sababu fursa nyingi zinapatikana kwa wadau hao ,nakuwaasa wasitoe fursa kwa kufahamiana bali kwa kila mtanzania anaye kidhi vigezo kulingana na Katiba, sheria na taratibu za nchi.

 

Aidha, Dkt. Chaula aliliambia Kongamano hilo kuwa, Wizara  imepokea maoni yote yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia  kazi kwa haraka, uaminifu na uadilifu mkubwa ili fursa zilizobainishwa namasuala mengine yaliyojadiliwa ambayo yanahitaji mkakati  wakidijitali, kwa kushirikiana na wadau mkakati huo utaandaliwa na kutekelezwa kwa wakati.

 

Naye Mhadhiri kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),Dkt. Moses Mwasaga amesema kuwa matumizi stahiki ya simu janja yatawezesha watu wengi zaidi kuingia na kushiriki kwenye uchumi wakidijitali kwa kupata huduma mbalimbali na kutengeneza ajira kama ilivyokupitia mfumo wa miamala ya fedha kupitia simu ya mkononi, ambapo watu wengi wameweza kujiajiri kama mawakala wakutoahuduma hiyo muhimu ambayo hapo awali ilikuwa ikitolewa na benki pekee.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: