IMG-20201011-WA0102
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akizungumza na timu za Kisayansi Kata ya Nshambya
IMG-20201011-WA0015
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha na timu ya Kisayansi ya Kata ya Kahororo
IMG-20201011-WA0005
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Kisayansi Mtaa wa Kisindi kata ya Kashai
IMG-20201011-WA0007
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akiwa kwenye timu ya pamoja na timu ya Kisayansi Kata ya Nshambya na Mgombea Ubunge alifika kusalimia ,Adv Byabato
IMG-20201011-WA0002
TIMU ya Kisayansi ya Mtaa wa Kashenye Kata ya Kashai
IMG-20201011-WA0107
TIMU ya Kisayansi ya Wazee Mashuhuri kutoka Kijiwe cha Senet,Soko Kuu na Bukoba  wakiwa na 

Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira
 
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira amekutana na Timu za Kisayansi zote nne alizoziunda kutoka mitaa 10 ya Jimbo la Bukoba Mjini ambayo yeye ni Mlezi wa Uchaguzi wa CCM. Timu hizi zina wajumbe wa kimkakati na uwakilishi wa makundi yote muhimu.

Lengo la kukutana ilikuwa kujitathimini na kupelekea mipango ya kisayansi itakayo wezesha ushindi wa kishindo wa CCM kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani Octoba 28 mwaka huu.

Akizungumza Neema alisema ili kufanikisha lengo kuratibu ushindi kwa CCM kwenye mitaa 10 kwa kutumia ubunifu aliamua kuunda timu za kisayansi 4 kutoka makundi yote muhimu .

“Timu hizo zina jumla ya watu 140 wa kimkakati ambao kwa kushirikiana na Lugangira wanaratibu kazi ya kisayansi kwa maeneo ya kisayansi na Octoba 9 na 10 mwaka huu nimekutana na timu zote nne kwa lengo la kujitathamini” Alisema

 
Pamoja na Timu hizi 4 za Kata, Lugangira pia aliunda Timu ya Kisayansi ya Wazee 15 Mashuhuri kutoka Kijiwe cha Senet, Soko Kuu Bukoba Mjini ambao pia alikutana nao tarehe 8 Oktoba 2020 na kupata tathmini ya majukumu ya kisayansi aliyowakabidhi.

Aidha alisema pia lengo lingine la Mikutano hii ilikuwa ni kuweka mipango ya kisayansi itakayopelekea ushindi wa kishindo wa Chama cha Mapinduzi kwa ngazi ya Rais, Ubunge na Udiwani katika uchaguzi huo.

 
“Kwa Kampeni yetu ya Kisayansi lazima Wilaya ya Bukoba Mjini ichukue nafasi yake ya kuwa sebule ya Mkoa wa Kagera", Alisisitiza Lugangira.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: