NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Laban Kihongosi amewataka wanafunzi wakike kutambua kuwa wana wajibu wa kusoma kwa bidii na kutokukubali kurubuniwa kwani wanatakiwa kuja kulisaidia taifa hapo baadae katika uwakilishi wa wanawake.


Kenan alitoa rai hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike wilaya ya Arusha ambapo aliwaeleza watoto wa kike kujaribu kukataa vishawishi na kufuata ushauri wa wazazi, walezi pamoja na walimu wao ili miongoni mwao waweze kupatikana viongozi.


Aidha alikemea vitendo vya ukatili vinavyoendelea katika jamii dhidi ya watoto ikiwemo ukeketaji ambapo madhara yake yanatokea  wanapofikia utu uzima, mimba za utotoni na ubaguzi katika familia na jamii kwa ujumla.


“Mila hizi potofu tuseme inatosha sasa na tuachane nazo  na ubaguzi wa kijinsia pia kwani mtoto wa kike na wakiume wato kwa pamoja wanaweza hivyo wasibaguliwe ili wafikie ndoto zao,” Alieleza Kenan Kihongosi.


Naye afisa ustawi  wa jamii wa halmashauri ya jiji ,Nivoneia  Kikaho alisema vitendo vya kikatili vimeongezeka kutokana na baadhi ya familia ,walezi na wazazi kutokutoa Ushahidi katika mahakama hivyo watu wajitokeze kufichua vitendo hivyo vinamnyima mtoto haki yake.


“kesi za Watoto huchukuliwa kwa namna ya pekee ikiwa wazazi na walezi wakitoa ushirikiano kwani kuna baadhi ya wazazi huwashawishi Watoto wa kike katika maswala ya ngono hali ambayo humfanya mtoto huyo kutopenda shule kutokana na vitendo anavyofanyiwa,”alisema Kikaho.


Mtaalamua wa kuzuiya ukatili wa kijinsia na elimu kutoka shirika la World education  Grece Muro aliwataka walimu kutokuwa wakali kupita kiasi badala yake wajenge ukaribu na watoto ili kuweza kujua changamoto zinazowakabili kuweza kuzitzfutia ufumbuzi lengo likiwa ni kuwasaidia kufikia ndoto zao.


Pia alieleza kuwa takwimu bado zinaonesha kuna vitendo vya kingono baina ya walimu wa kiume na wafunzi jambo ambalo linapelekea kupata ujauzito na kukatisha ndoto za watoto katika kufikia malengo yao.




“Mtoto anapofanyiwa ukatili, anashindwa kupata usikivu, anajisikia na kuona kama hatakiwi  hali inayomfanya kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao n ahata kutoroka na kuacha shule kabisa” alisema Grece Muro.


Kwa upande wa mwakilishi wa watoto wa kike jiji la Arusha Brenda Malya kutoka shule ya sekondari ya Arusha Day alieleza kuwa bado vitendo vya ukeketaji na ubakaji vinaendelea katika jamii  pamoja na kuwepo kwa sharia kali hivyo wanaiomba serikali ya wilaya hiyo kuunda tume itayoshughulikia vitendo hivyo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: