Monday, 21 September 2020

WAZIRI BITEKO APONGEZA UTENDAJI KAZI WA TUME YA MADINI


Waziri wa Madini, Doto Biteko amepongeza  utendaji kazi wa Tume ya Madini uliopelekea kuvuka kwa lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2019 – 2020.

Waziri Biteko ametoa pongezi hizo leo tarehe 21 Septemba, 2020 kwenye ziara yake katika banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji cha Bomba Mbili mjini Geita.

“Nashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya katika kuhakikisha Serikali inavuka lengo kwenye ukusanyaji wa maduhuli,” amesema Waziri Biteko.


No comments:

Post a comment