William Ndilla. Sumve .
Mwanza,Tanzania.
September 18,2020.

Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020 ilianisha eneo la Usafirishaji wa Anga Kama eneo la kupewa Kipaumbele hili kuweza kuchochea Ukuaji wa Uchumi.

Uwekezaji Mkubwa wa Kununua Ndege ulifanyika Chini ATCL na kulifanya Anga la Tanzania lianze tena Safari za Ndege za Ndani ambazo Soko lake lilikuwa limeshatekwa na Kampuni binafsi za Ndege Kama Fast Jet na Precision Air.

Kwa kutambua hilo Serikali ya AWAMU ya tano Chini ya Dkt John Magufuli iliamua Kuanza na Uwekezaji wa Kununua Ndege na baadae kuzikodisha kwa ATCL.

Jukumu la Pili Kubwa ilikuwa ni Utanuzi wa Miundombinu ya Usafirishaji wa Anga ikiwepo Uwekezaji wa Rada Kubwa na za kisasa Katika Mikoa ya Mbeya,Mwanza,Dar es salaam na Kilimanjaro.

Pia jitihada za Kuendelea na Ujenzi na Utanuzi wa Viwanja vya Ndege vya Mwanza,Mbeya,Dodoma,Chato,Songea,IRINGA na Maeneo mengineyo ziliendelea kwa kasi Kubwa.

Msije kusema ni Ndilla kaandika , Bali ni Pamoja na Ilani ya CCM kuainisha Umuhimu wa Kutambua  Maeneo yenye faida za Kigiografia ambayo Kama yangetumika yangeweza kuongeza Mapato Pamoja na Shughuli za Kiuchumi Katika Nchi.

Uwepo wa Bandari ya Dar,Mtwara,Nyasa,Tanganyika na Victoria Ulipewa Kipaumbele kwa Kuwekeza Katika Vyombo vya Usafiri hili Kuwezesha Biashara baina ya Nchi na Maeneo Fulani Fulani.

Katika kutambua Maeneo ya MKAKATI ya Kigiografia,Eneo la Mkoa wa Geita lilikuwa Moja wapo la eneo ambalo lilipewa Jicho la tatu kutokana na fursa Mbalimbali za Kiuchumi na za Kigiografia Katika eneo husika hili liweze Kuchangia kikamilifu Katika kuongeza Pato la Taifa.

UKWELI NA NGUVU ZA KIUCHUMI ZA  MKOA WA GEITA.

Geita ni Mkoa Uliotokana na Kumegwa kwa Mikoa Mitatu yaani Mwanza,Kagera na Shinyanga na kuweza kuzaa Wilaya tano ikiwemo Wilaya ya Chato. Mkoa huu Ulianzishwa Mwaka 2012.

Wakazi wa Mkoa wa Geita shughuli Zao Kubwa ni Kilimo,Uvuvi,Uchimbaji Madini na Ufugaji na Utalii. Mkoa wa Geita Umebatizwa Jina la Utani la "Golden State"yaani Jimbo la dhahabu Kutokana na Uwepo wa dhahabu nyingi Chini ya Ardhi ya Geita.

Ilani ya CCM ya Mwaka 2020/2025 Ukurasa wa 25 kipengele Cha 28, Chama Cha Mapinduzi kinaielekeza Serikali yake Kutumia fursa ya Kigiografia Katika kuiletea Tanzania Maendeleo.

Moja ya eneo ambalo lilishaainishwa ni eneo la Mkoa wa Geita na kumua kujenga Uwanja wa Ndege Wa Kimataifa wa Chato hili kuweza kuifungua Geita kibiashara na Nchi zingine Kama DRC,Rwanda,Uganda na Burundi ambazo hazina Lango la Bahari"Land locked Countries.

Mkoa wa Geita ambao Umekuwa na Shughuli Kubwa za Uzalishaji wa Dhahabu,Utalii,Uvuvi na Ufugaji hivyo Kufanya Uwepo wa Umuhimu wa Uwepo wa Usafiri Bora wa Anga hili kuweza kuchochea Shughuli za Kimaendeleo na Kiuchumi Katika Mkoa huo na Mikoa Jirani.

Kuchochea Utalii,Biashara na Uwekezaji.Uwepo wa Mbuga ya Burigi-Chato pia kuliongeza uwepo uhitaji wa kuifungua Geita na Usafiri wa Anga kwa hiyo Uwanja wa Chato Ukawa hauepukiki.

Uwepo wa Masoko na Machimbo Makubwa na Biashara Kubwa ya Madini Ulikuwa lazima Uendane na Uwepo wa Usafiri wa haraka na Uhakika wa Ndege.Gharama Kubwa za Usafirishaji wa Mizigo toka Mwanza kuja Geita na Kutoka Geita kuja Mwanza pia kulichochea Uhitaji wa haraka wa Uwanja wa Kimataifa wa Chato.

Ilionekana Usafiri wa Moja kwa Moja kwa Wawekezaji toka Nje ya Nchi kuja Maeneo ya Machimbo au Uwekezaji ya Geita ingekuwa ni nafuu Kiuchumi na kupunguza gharama za Usafiri ambazo Muekezaji alikuwa anazibeba Kutokana na kutakuwepo kwa Uwanja wa Ndege wa Geita.

Katika Mazingira Kama haya,Kiwanja Cha Ndege Cha Chato kilikuwa hakiepukiki Jana,Leo na ata Kesho.

Uingizaji wa Mitambo ya Kuchimba Madini, technolojia zingine Pamoja na fedha Kutoka Nchi Washirika wa Biashara Ungekuwa rahisi Kama Kungekuwepo na Ndege za moja kwa moja toka Mataifa ya Ulaya Mpaka Maeneo ya Uwekezaji.

KWANINI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA CHATO ULIENDA KUJENGWA WILAYANI CHATO?

Jibu ni rahisi Sana na nianze kwa Kusema Kwamba ni Utaratibu wa Kawaida kwa Viwanja vya Ndege Vyote duniani kujengwa Nje ya Miji na Sababu zipo nyingi za Kiusalama, kiafya na Kimkakati.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Chato Upo Kilometa 20 toka Makao Makuu ya Mkoa wa Geita.Huu Ndio "Utamaduni" wa  Ujenzi wa Viwanja Vya Ndege Vyote duniani.


Angalia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe Mbeya, Upo Kilometer Kumi Kutoka Jijini la Mbeya.

Angalia Uwanja wa Ndege wa  KIA  Kilimanjaro, Upo Umbali wa Kilometa Zaidi ya 20 ya yalipo Makao Makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro. Uwanja huu Upo Katika Wilaya ya HAI.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Msalato Dodoma nao Upo Zaidi ya Kilometa 10 toka Dodoma Mjini.

Kupeleka Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato kwenda Katika Wilaya ya  Chato baadala ya Kuujenga  Geita Mjini Ulikuwa ni Uamuzi wa Wataalam wa Masuala ya Anga na Sio Uamuzi wa Mh. Rais John Magufuli.

Ni Mjinga tu Ndio atakayesema Uwanja wa Ndege wa Chato ulipelekwa Chato kwa Sababu Ndio Nyumbani Kwao na Rais na ameshasema Yeye akishastaafu basi ataenda kuishi Mkoani Kagera.

Kwa vile alijua kuwa ataenda Kuishi Kagera kwanini sasa aamua kujenga Uwanja Mkubwa wa Ndege wa  Chato na Sio Kagera?

UWANJA WA NDEGE WA CHATO UNA LENGA KUZIFUNGUA FURSA ZA UTAJIRI WA MKOA WA GEITA NA SIO KINGINE.

Uwanja wa Kimataifa wa Chato Una lengo la Kiuusaidia Uwanja wa Ndege wa Mwanza Uweze kushughulika na Mambo Mengine huku Uwanja wa Kimataifa wa Chato Ukiwa Ndio wa kubeba Jukumu la kuwahudumia Wafanyabiashara wa dhahabu,Wavuvi,Wagema Asali Pamoja na Watalii waliopo Katika Mkoa wa Geita.

Kwa asiyejua fursa zilizopo Katika Mkoa wa Geita anaweza akabeza Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Chato Sababu ya kukosa taarifa sahihi za Serikali na za Kimkakati.

Ukisoma "Geita Regional Investemei Guide" Unaweza angalau ukaelewa Nini ninachotaka Kusema hapa kuhusu Uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Chato Kama Uwanja Mkakati Katika eneo hili lililo na Kila Aina ya Utajiri wa Kilimo,Uvuvi,Utalii na Madini.

Sababu Zifwatazo zinajibu Swali la kwa Nini Ni muhimu Zaidi kuwa na Uwanja wa Ndege wa Chato wakati huu Kuliko huko nyuma.

Uwepo wa Soko Kubwa la dhahabu Katika Mkoa wa Geita ambapo Zaidi ya asilimia 60 ya dhahabu Yote  inachimbwa hapa Nchini inatoka Mkoa wa Geita.

Hii ina Maana gani?,Hii ina Maana kwamba Mahitaji ya Usafirishaji wa Dhahabu Kutoka hapa kwenda Mataifa ya Nje ni Makubwa na Ukizingatia Umbali wa Kutoka Geita Kwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza kunapoteza muda na Kuongeza gharama za Usafirishaji.

Pia Uwepo wa Masoko ya dhahabu katika Miji ya Geita Mjini na Katoro Unahitaji Uwepo wa Ndege za Kusafirisha Mizigo ya Wawekezaji kupitia
Uwanja wa Ndege wa Chato.

Uwanja wa Ndege wa Chato Ndio utakuwa Mkombozi kwa Usafirishaji wa bidhaa zinazopatikana Katika Mkoa wa Geita Kama Samaki,Asali,Watalii,na Madini.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato Umeongezeka Uwepo wa ajira za moja kwa Moja na zisizo za moja kwa moja.Ajira za kwenye Ndege na Uwanja wa Ndege kwa jumla.

Uwanja wa Chato Ulilenga pia kuifungua Geita na kuweza kufanya Biashara Katika Sekta ya Utaliii kupitia Uwepo wa Kisiwa Cha Lubondo na Uwepo wa Utalii wa Kuvua Samaki"Sports Fishing".

Kuongeza Mtandao wa Safari za  Ndege za Not ya Tanzania  na Kuongeza Safari za Moja kwa moja toka Mataifa ya Nje kuja Tanzania nayo ni Yao fursa kwa Mkoa Geita.

Propaganda za Mgombea wa URAIS wa Chadema hazina mashiko Wala hoja za Kiuchumi Zaidi ya kueneza Chuki dhidi ya Serikali.

Ni wazi kuwa Ujenzi wa Uwanja huu na Viwanja Vingine Nchi Nzima unaenda kuongeza na kufungua fursa za Kiuchumi na kuongeza Mapato ya Serikali ya AWAMU ya Tano Chini ya John Pombe Magufuli.

Kama Mgombea URAIS  wa Chadema hajui Wala Mipango ya Serikali hii ya awamu ya tano ni Bora akae kimya.

Mgombea huyu anapaswa kujikita Katika kuitangaza Ilani ya Uchaguzi  ya Chama Chake na Nini anataka kuwafanyia Watanzania.Kuongelea Ujenzi wa Uwanja wa Chato ni Kuendelea kuinadi Ilani ya CCM.

William Ndilla
Sumve, Mwanza, Tanzania.
+255759929244
Share To:

msumbanews

Post A Comment: