MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza wakati alipofanya ziara yake ya kutembelea miradi ya maji kujionea namna unavyotekelezwa eneo la Horohoro Mkinga mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais Dkt Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu zaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani kushoto ni  Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akieleza jambo wakati wa ziara hiyo kuhusu mradi huo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati alipofanya ziara kwenye mradi wa maji wa Horohoro
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika wakati alipotembelea mradi huo kulia ni Mhandisi Upendo Lugongo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika wakati alipotembelea mradi huo kulia ni Mhandisi Upendo Lugongo anayefuatia kwa nyuma ni Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga Joseph Sura

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameitaka Mamlaka ya Maji Safi,Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuimarisha maeneo yanayotorosha maji kwenye bwawa la maji la Hohorohoro wilayani Mkinga.

Shigela aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara yake ya kutembelea miradi ya maji kujionea namna unavyotekelezwa ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais Dkt Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu zaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani

Ambapo mradi huo unatekelezwa na Mamlaka Tanga Uwasa  una thamani ya milioni 360 upo kwenye asilimia 85 na mmehaidi asilimia 15 zilizobakia mtakamilisha ifikapo mwisho wa mwezi Septmeba mwak 

“Ndugu zangu Tanga Uwasa mnafanya kazi nzuri sana lakini hakikisheni mnatenga fedha kwa ajili ya kuimarisha maeneo yanayotorosha maji kwenye bwawa la maji la Hohorohoro wilayani Mkinga”Alisema

 “Lakini pia Bwawa hili kwa kweli halitoshelezi kama mnavyoona maji yamepungua sana nimeelezwa kupitia fedha mlizonazo za PFR mhakikishe mnatenga fedha kwa ajili ya kuimarisha maeneo yanayotorosha maji”Alisema

Hata hivyo aliwataka pia kuanza upanuzi wa bwawa hilo kupitia force akaunti ili mvua zitakaponyesha wawe na uhakika wa kuhifadhi maji huku akieleza umuhimu wa kuhakikisha wanaongeza vilula vya kuchotea maji wananchi kutokana na kwamba hivi sasa vipo vichache ili kuwaepusha kujazana eneo moja.

“Nizipongeze mamlaka za Maji Mkoa wa Tanga kwa kuona umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo  maelekezo ya Rais Dkt Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu zaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani”Alisema RC Shigela.

Hata hivyo alionyeshwa kufurahishwa na hatua ya mradi huo ilipofikiwa huku akihaidi kwenda kukagua kuona kama maji yanatoka Octoba 15 kuja kuona kama maji yanatoka eneo hilo la Horohoro.

“Kwa sababu eneo la Horohoro kwetu sisi ni eneo la kimkakati kwa sababu tunataka iwe ndio iwe habu ya biashara kati ya Kenya na Tanzania watu wanaotaka kufanya biashara wafike eneo hilo watapata bidhaa kutoka Kenya na Tanzania”Alisema

Awali akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema Tanga Uwasa wanajenga mradi huo kwa kushirikiana na Ruwasa na umefikia asilimia 85.

Mhandisi Hilly alisema wanategemea mpaka ifikapo ndani ya mwezi wa Septemba na Octoba kazi za msingi zitakuwa zimekamilika na wananchi kuendelea kuhudumiwa kama ilivyopangwa tangu mwazo pamoja na na kituo cha Forodha cha Horohoro mpakani.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo  alisema mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa kwa mwisho wa mwezi wa Septemba mwaka huu watu waanze kunywa maji lakini kwa maboresho ambayo aliwaagiza kuyafanya watahakikisha yanafanyika kwa fedha kidogo walizopokea.

Alisema ili wananchi wanapata maji safi na salama ikiwemo kuhakikisha bwawa hilo linauwezo mkubwa wa kutunza maji kwa kufanyia maboresho kwenye maeneo yaliyoonekana na changamoto.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: