Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) na Chuo cha Madini Dodoma( MRI) wameendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji  Bomba Mbili Mjini Geita.

Taasisi  nyingine zilizopo chini ya Wizara ya Madini  zinazoshiriki katika maonesho hayo ni pamoja na Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Mgodi wa STAMIGOLD.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: