Wednesday, 2 September 2020

MAJALIWA AMUAGIZA DC NA MKURUGENZI KUTENGENEZA 'AMBULANCE' MARA MOJA.
Na Woinde Shizza ,Arusha

Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye pia Ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kasimu Majaliwa amemtaka mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele  pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Stephen Ulaya kukarabati haraka magari ya kubebea magonjwa matatu  ambayo yameharibika kwa sasa.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa kampeni za Ubunge   katika Jimbo Monduli Majaliwa alisema kuwa Serikali imetoa magari Hayo ili Kuhakikisha kuwa wananchi,wanaletewa huduma za afya kwa katika vijiji  hivyo Ni vyema wanatengeneza mapema  ili wananchi waweze kupata huduma.

Aidha alisema kuwa Serikali ilileta magari ya kubebea wagonjwa matano lakini amesikia magari mawili tu ndio yanafanya kazi kitu ,hivyo alimuagiza mkurugenzi afanye haraka magari Hayo kukamilika  .

Alisema kuwa kila mtu anajua kazi zilizofanywa  na  Serikali inayoongozwa Chama Cha mapinduzi ,katika kipindi Cha uongozi wa miaka mitano iliopita Ambapo alisema kwa kutekeleza ilani ya Chama Cha mapinduzi ,Serikali yetu imeweza kuleta maendeleo pamoja na kuing'arisha nchi yetu 

"Tumeweza kujenga vituo vya afya 498 zenye huduma zilizokamilika ikiwemo huduma za upasuaji ,tunatoa huduma pia ya mama na mtoto ,lakini pia mkitupa ridhaa tunampango wa Kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na kituo Cha afya,pia tunampango wa kuboresha swala la elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari katika hili napenda niseme tukipita katika kipindi hiki ni lazima kila mwananchi atakaezaa mtoto akasome sio ombi bali ni lazima"alisema Majaliwa

Kwa upande wa mifugo na uvuvi tumejipanga Kuhakikisha kila mfugaji anafuga na anapata faida na mkulima analima na kupata faida na ndio maana tumewatoa maafisa mifugo na maafisa kilimo  ofisini na tumewaleta ukuvijiji kwenu ili wawasaidie.

"Nimesimama  hapa kumuombea Kura Rais wetu pamoja na wabunge na madiwani wapeni Kura ili tukaweze kutekeleza ilani Hii mpya ya Chama Cha mapinduzi yenye kurasa 303 na tunauhakika tutaitekeleza zaidi Ile ya awali 2015/2020"alibainisha Majaliwa

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Fready Lowasa alisema kuwa iwapo ata pita Ndani ya siku 100 ataanza na kutatua mgogoro wa muda mrefu baina ya wakulima na wafugaji uliopo monduli juu pamoja na changamoto zingine zote zilizopo katika Wilaya ya Monduli.


Kwa upande wa katibu wa CCM mkoa wa Arusha Mussa Matoroka alisema alisema kuwa kwa upande wa Jimbo la Monduli Asilimia kubwa ya madiwani wamepita bila kupigwa .

No comments:

Post a Comment