Wednesday, 23 September 2020

DKT. NDUGULILE AZINDUA MASHINA YA CCM KATA YA VIJIBWENI


Mgombea ubunge jimbo la Kigamboni Daktari @faustine_ndugulile amezindua mashina mbalimbali ya @ccmtanzania na Jumuiya zake katika mitaa kadhaa ndani ya kata ya Vijibweni.

Dkt.Ndugulile amezindua mashina katika Mitaa ya Chaboko,Upendo na Mkwajuni ambayo ni Shina la Kibaoni,Msufini,Mzee Mtula na Upendo.

Aidha Dkt.Ndugulile ametembelea makundi mbalimbali maalum ya waanchi wakiwemo Vijana waendesha Bodaboda,akina Mama ntilie,wauza mbogamboga za majani,wafanya biashara wadogowadogo wa maduka ya bidhaa mbalimbali na Vijana wa mchezo wa soka katika mtaa wa Kibene na katika makundi yote yote hayo ameweza kuwasikiliza na kuchukua changamoto zao mbalimbali wanazokutana nazo ilikusudi kuzifanyia kazi kwa haraka mara baada ya Oktoba 28 mwaka huu kumpa kura za ndio kama walivyomuahidi.

"Vijibweni tunataka kuweka soko na kuna maeneo mawili ambayo tunayatazamia likiwemo eneo la kule kwa Mkorea na eneo la NSSF tunafanya mazungumzo katika kuomba kupata eneo moja wapo kati ya hayo kujenga soko" Dkt.Ndugulile.

"Nawashukuru sana vijana kwa kunipa fursa ya kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huu mnatupa matumaini makubwa sana sisi wagombea,kata ya vijibweni ina wapiga kura zaidi ya 30 elfu na wengi ni Vijana naomba tusipige tuu iyenaiyena bali tutafute kura kwa wingi na ni kwa kuyasema yale yote ambayo serikali ya awamu ya 5 imeyatekeleza katika ngazi zote" Dkt.Ndugulile.

"Hapa vijibweni 2015 mlichanganya mkafanya madudu na matokeo yake mmeona hakuna maendeleo ya maana hapa,huu ni wakati wa kujifunza naombeni kura yenu ya Ndiyo kwangu udiwani,kwa Ndugulile ubunge na kwa Mhe.Rais Magufuli kuendelea katika nafasi yake" Zachari Mkundi (White) Mgombea udiwani kata ya Vijibweni.

#Vijibweni
#KigamboniMpya

No comments:

Post a comment