NA HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Ilala   Ng'wilabuzu Ludigija  amemaliza mgogoro wa shule ya Kisasa  Gurukwalala Kata ya Gongolamboto halmashauri ya Ilala kwa kuigawanya sehemu mbili ,shule ya Msingi ya kawaida na English Medium.

Sakata hilo limetokea leo katika kikao cha wananchi eneo la Gurukwalala  wakati wa kusikiliza kero za wananchi ambapo wananchi wa kata hiyo walimpokea Mkuu wa wilaya hiyo kwa kilio cha shule kufuatia shule yao kupisha mradi wa Serikali    Reli ya kisasa.

" Serikali yenu ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ni sikivu mikakati yake kuwapatia elimu bure watanzania wote  watasoma mpaka kidato cha nne  " alisema Ludigija

Ludigija alisema  serikali baada kuvunja shule iliyokuwa Gurukwalala kupisha mradi wa Reli ya Kisasa imenunua eneo lingine imejenga shule ya kisasa madarasa 23 ,kati ya madarasa hayo madarasa 10 yatatumika kwa shule ya kawaida na mengine English Medium.

Alisema  wanafunzi wa pembezoni mwa manispaa ya Ilala na watoto kata za jirani watasoma Gongolamboto shule ya English Medium.

Ludigija alisema watoto wote watasoma katika shule hiyo  amna mtoto atakaye soma mbali na kata ya Gongolamboto.


Kwa upande wake Afisa DAWASA Mkoa wa Ukonga  Melkiard Lyamuya  alisema Ukonga kuna utekelezaji wa miradi mkubwa wa Maji  wa Kisarawe Pugu unatarajia kukamilika Desemba mwaka huu utakapokamilika changamoto za maji safi ya DAWASA  baadhi ya kata jimbo la ukonga litakuwa limeisha.


Naye Afisa TARURA Wilaya ya Ilala Slilo Joseph alisema kwa mwaka wa fedha 2021 katika Jimbo la Ukonga  TARURA wamepanga kutengeneza KM 100 ili kutatua kero kwa wananchi.

Aidha Joseph alisema kuna barabara zingine zitafikiwa lami kupitia mradi wa DMDP baadhi ya barabara hizo Majohe,Moshi Baa,Pugu Stesheni.

Alisema serikali ya awamu ya tano ni sikivu ipo karibu na wananchi kutatua kero mbalimbali .

Mwisho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: