Friday, 21 August 2020

MAN FONGO : NDOTO YANGU KUFANYA KAZI NA DIAMOND PLATNUMZ


Msanii wa muziki wa Singeli, Man Fongo amesema kuwa ndoto yake, siku moja kufanya wimbo na boss wa WCB, Diamond Platnumz.

Man Fongo ameyasema hayo leo Ijumaa Agosti 21, 2020 katika kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM alipokuwa anatambulisha wimbo wake mpya aliomshirikisha Mzee wa Bwax unaitwa 'Matapeli'.

Mtangazaji wa kipindi hiko, Dida alimuuliza Man Fongo 'Wasanii wengi wa singeli wanafanya kazi na wasanii wa bongo fleva wewe unatamani kufanya kazi na msanii gani.'

Man Fongo alijibu kwa kusema "Simba, Diamond Platnumz, ndiyo ndoto yangu kubwa siku moja kufanya nae kazi"

"Kwa upande wa singeli msanii ambaye tamani kufanya nae kazi Msaga Sumu, lakini itatokana na ushauri wa watu wangu na uwitaji wa msanii katika wimbo husika, kwani hata huu wimbo wangu mpya nilifanya mwenyewe lakini wakaona hapa anafaha kukaa Mzee wa Bwax" alisema Man Fongo.

No comments:

Post a Comment