Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akielezea jambo wakati wa kikao chake na Makamishna wa Uhifadhi nchini, kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akisisitiza kuhusu umuhimu wa kupitia vema Miundo ya Taasisi za Uhifadhi ili kuliwezesha jeshi hilo kutenda kazi zake kiutaalam zaidi na kwa ufanisi mkubwa huku Taasisi za Uhifadhi zikizingatia kuimarisha Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu na kudhibiti ujangili.

kikao hicho cha kujadili na kupitia Miundo ya Taasisi ( Organization Structure) ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, kimehudhuriwa na Makamishna wa Uhifadhi wa Taasisi za Uhifadhi za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Hifadhi za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.


TAZAMA MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA.



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akifuatilia kwa umakini michango ya wajumbe wakati wa kikao chake na Makamishna wa Uhifadhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akisisitiza kuhusu umuhimu wa kupitia vema Miundo ya Taasisi za Uhifadhi ili kuliwezesha jeshi hilo kutenda kazi zake kiutaalam zaidi na kwa ufanisi mkubwa huku Taasisi za Uhifadhi zikizingatia kuimarisha Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu na kudhibiti ujangili Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Maurus Msuha

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akisisitiza kuhusu umuhimu wa kuzipitia vema sheria za Uhifadhi ili kuwezesha utekelezaji wenye ufanisi utakaoleta matokeo chanya na ya haraka katika Jeshi la Uhifadhi huku Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akifuatilia vema maelezo ya Naibu Katibu Mkuu Dr. Allan Kijazi.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi- Rasilimaliwatu Witness Shoo ( aliyesimama ) akijibu swali lililohitaji ufafanuzi kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Kanali Martin Michael Kilugha ( aliyevaa uniform za JWTZ wa tatu kutoka kushoto kwa Witness Shoo.
Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dkt. Fredy Manongi, akisisitiza kuhusu utekelezaji wa sheria kwa watumishi wa Jeshi la Uhifadhi ili kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya katika nyanja zote.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA, William Mwakilema akifafanua jambo wakati wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kulia ni Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) ni Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma Saidizi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Emmanuel Wilfred.
Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo akifafanua kuhusu masuala muhimu ya kuzingatia katika suala zima la utekelezaji wa Jeshi la Uhifadhi wenye matokeo chanya.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini, wakifuatilia kwa ukaribu mada zilizokuwa zikitolewa kwenye kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini, wakimsikiliza kwa umakini Naibu Katibu Mkuu Dkt. Allan Kijazi wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wakuu wa Taasisi za Uhifadhi Tanzania, wakifuatilia kwa ukaribu kikao cha kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki
Washiriki wakifuatilia kwa umakini mkubwa, kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini, kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Kanali Martin Michael Kilugha ( aliyevaa uniform za JWTZ , kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi - Usimamizi wa Sheria na Mikakati ya Ulinzi na Usalama, John Nyamhanga ( kulia) wakifurahia jambo kufuatia michango ya wajumbe wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Taasisi za Uhifadhi Tanzania, kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akiongoza kikao cha kujadili na kupitia Miundo ya Taasisi  ( organization structures ) ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: