Monday, 31 August 2020

Katibu Mkuu Afungua Kikao cha kujadili Hali ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Maeneo yaliyokasimishwa kwa Taasisi za Wizara.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki akitoa Hotuba ya Ufunguzi katika Kikao cha kujadili Hali ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Maeneo ya Malikale yaliyokasimishwa kwa Taasisi za Wizara kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS ) Kituo cha Mbegu za Miti Morogoro. Aliyekaa Kushoto kwa Katibu Mkuu, ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale, Dkt. Fabian Kigadye na (kulia) ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi na teknolojia - Idara ya Mambo ya Kale, Dr. Bwasiri Emmanuel.
 
 Washiriki wa Kikao cha Kujadili Hali ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Maeneo ya Malikale yaliyokasimishwa kwa Taasisi za Wizara, wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Ufunguzi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki (Hayumo pichani) kwenye ukumbi wa  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS) Kituo cha Mbegu Morogoro.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Malikale, Dkt. Fabian Kigadye akizungumza katika Kikao cha kujadili Hali ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Maeneo ya Malikale yaliyokasimishwa kwa Taasisi za Wizara  kilichofanyika katika  Ukumbi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS ) Kituo cha Mbegu za Miti Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga (katikati) pamoja na Mtaalam wa Malikale Prof. Audax Mabula mara baada ya ufunguzi wa Kikao cha kujadili Hali ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Maeneo ya Malikale yaliyokasimishwa kwa Taasisi za Wizara kilichofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS ) Kituo cha Mbegu za Miti Morogoro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kikao cha kujadili Hali ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Maeneo ya Malikale yaliyokasimishwa kwa Taasisi za wizara kilichofanyika jana mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment