Friday, 21 August 2020

HAJI MANARA : YANGA KUMBEBA KIONGOZI WAO TUKIO LA HOVYO KABISA


BAADA ya jana Agosti 20 mashabiki wa klabu ya Yanga kumbeba Mkurugenzi Mwekezaji kutoka Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said wakati wa mapokezi ya wachezaji wapya wawili Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko kutoka AS Vita ya Congo.

Msemaji wa Simba SC, Haji Manara ameibuka na kusema kuwa kitendo hiko ni cha hovyo kabisa.

Akizungumza katika moja ya chombo cha radio mtandaoni, Manara amesema anawapenda mashabiki wa Yanga kwa kuwa ni watulivu ila kitu cha kumbeba kiongozi wao juu ni tukio la hovyo.

"Kitu pekee ambacho nakipenda Yanga ni kuwa wana moyo wa chuma, ni wavumilivu hasa, kwani matokeo yale wanayopata huku wanambeba kiongozi wao juu ni tukio la hovyo kabisa lile" alisema Manara.

No comments:

Post a Comment