Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Katibu Tawala mkoa huo Richard Kwitega akifungua Mafunzo ya Wadadisi wa Sensa ya Kilimo Mifugo na Uvuvi iliyondaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mikoa ya Kanda ya kaskazini ikiwa ni muendelezo wa mafunzo hayo kwa nchi nzima yaliozinduliwa na Naibu Waziri wa Kilimo Jijini Mwanza mapema mwishoni mwa wiki yenye lengo la Zoezi la Sensa ya Kilimo Uvuvi na Mifugo itakayofanyika kwa miezi miwili ya August na September mwaka huu leo jijini Arusha katika ukumbi wa Shele ya Sekondari Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Afisa Takwimu Muandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Robert Kasililwa akisoma taarifa ya mafunzo hayo mbele ya mgeni rasmi katibu tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa sensa ya kilimo mifugo na uvuvi itakayofanyika kuanzia mwezi ujao hadi mwezi wa september mwaka huu kwa kipindi cha siku 45 hadi 60 likiwa ni zoezi la sensa ya kilimo 

Wakufunzi wa semina hiyo wakifuatilia kwa karibu hotuba ya mgeni rasmi Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa sensa ya kilimo mifugo na uvuvi mapema leo jijini Arusha 

WAWAKILISHI na wadadisi kutoka mikoa ya Arusha Manyara Kilimanjaro na Tanga akifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ya sensa ya kilimo iliyofunguliwa na Katibu tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega hayupo pichani mapema leo jijini  Arusha

Meza Kuu kutoka kushoto ni Meneja wa Takwimu mkoa huo Leokadia Mtey akifuatiwa na Mgeni Rasmi Katibu Tawala mkoa huo Richard Kwitega akifuatiwa na Afisa mwandamizi kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu akifuatiliwa na Katibu Tawala msaidizi Uchumi na uzalishaji mali Hargeney Chitukuro wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa sensa ya kilimo mifugo na uvuvi iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Arusha jijini hapa

Wadadisi kutoka mikoa ya kanda yakaskazini wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa sensa ya kilimo mifugo na Uvuvi inayoendela kwa siku tatu  jijini hapa maepama leo jijini Arusha

WADAU wa mafunzo ya wadadisi wa sensa ya kilimo mifugo na uvuvi wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mafunzo yao mapema leo jijini Arusha kama walivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema sensa ya  takwimu za Kilimo mifugo na Uvuvi itakayofanyika kuanzia mwezi ujao taarifa itakazokusanywa itaonyesha hali halisi ya sekta ya kilimo nchini na kuiwezesha serikali kupanga sera mipango kuimarisha na kuboresha hali za wananchi.

Kwitega ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya wadadisi wa sensa ya kilimo mifugo na uvuvi ya mwaka 2019/20 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini yalioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu inayofanyika jijini Arusha.

Alisema kuwa kwa ujumla umuhimu wa kilimo unafahamika na takwimu hizo zitaonyesha jinsi sekta hiyo inavyochangia katika pato la taifa kwani mwaka 2019 sekta hiyo imechangia pato la taifa kwa asilimia 26.6 huku upande wa mauzo ya nje asilimia 24.3 ya fedha za kigeni ilipatikana.

Aidha alibainisha kuwa tafsiri ya takwimu hizo kuwa mwaka huo wakulima tulizalisha zaidi tukavuna zaidi na kuuza zaidi huku wafugaji walifuga zaidi wakauza zaidi na wakazalisha zaidi hivyo hatuna budi kujivunia mchango wetu kwa sababu tunachangia katika kukuza maendeleo tunayoyaona sasa.

Alisema kuwa Wakati tukielekea kwenye sensa ya kilimo Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2019/20 hatuna budi kuwakumbusha na kusisitiza kuwa mafanikio niliyoyataja hapo awali yanatokana na matumizi ya matokeo ya sensa ya mwaka 2007/8 ambayo ilifanyika kwa ufanisi mkubwa kwa kuonyesha maeneo tuliofanikiwa na kupiga hatua kubwa maeneo yaliosogea kidogo na yenye changamoto nyingi ambayo hayakupiga hatua kabisa pamoja na mipango na sera tulizotumia kufanikiwa.

"Kama alivyoeleza awali mwakilishi wa Mtakwimu mkuu wa serikali mafunzo haya yatakuwa na sehemu mbili za nadharia na vitendo itahusu kujaza dodoso la wakulima wadogo na wakubwa pia dodoso la mashamba makubwa la jamii mbinu za udadisi na kutumia teknolojia mpya katika kukusanya Takwimu kwa matumizi ya vishikwambi kwa kufuta sheria ya Takwimu muwe makini wa kuchukuwa taarifa sahihi" 

Aliwataka kuanzia sasa tunapoitisha vikao vyetu kuhakikisha kuwa ujumbe wa sensa uwe wa kudumu katika mikutano yetu na wananchi tuelimishe na kuhimiza kutoa ushirikiano kwa wadadisi wakati wote wa zoezi hili linapofanyika na kwa upande wa wananchi wajibu wao mkubwa ni kushirikiana na wadadisi kwa kujibu maswali kwa usahihi na ufasaha bila ya kuficha ukweli wa taarifa.

Awali akiongea wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mtakwimu mkuu wa Serikali Afisa Takwimu Muandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Robert Kasililwa alisema kila mwananchi ashirikiane na wadadisi kutoa taarifa sahihi ili serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo itakayosaidia kuongeza wigo wa kupunguza umaskini wa wananchi.

Alisema mafunzo hayo kitaifa yalianza siku ya Jumamosi wiki iliyopita kwa jumla ya wadadisi 322 nchi nzima kupatia mafunzo ya matumizi ya teknolojia mpya ya ukusanyaji wa Takwimu kwa mfumo wa Vishikwambi na kuachana na mfumo uliopita wa matumizi ya karatasi unaogharimu fedha nyingi.

Alisema kuwa teknolojia ya kisasa ambayo itapunguza gharama za kukusanya na kuchakata takwimu  kwa kiasi kikubwa sana tofauti na sensa ya mwaka 2007/8 ambayo ilitumia takribani bilioni 10 huku sensa hii ya mwaka 2019/20 ikitumia pungufu bilion 6 kwa pande zote za Muungano Aidha matumizi hayo ya teknolojia hiyo itarahisisha upatikanaji wa takwimu kwa muda mfupi na ubora zaidi tofauti na huko nyuma.



Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: