Fredrick Lowassa  ambaye ni Mtoto wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amechukua fomu ya kugombea ubunge Monduli, mkoani Arusha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) .

Fredrick amechukua fomu hiyo leo Jumanne tarehe 14 Julai 2020, katika Ofisi za CCM wilayani Monduli, mkoani Arusha na kukabidhiwa na Katibu wa chama hicho Wilaya ya Monduli, Langael Akyoo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli, Langael Akyoo, leo Jumanne July 14,2020 amemkabidhi Fredrick Lowassa fomu ya kuomba ridhaa ya Chama hicho ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Monduli. Fredrick ni Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Share To:

Post A Comment: