Zifuatazo ndizo hamasa ya mafanikio ya mafanikio unazoaswa kuzifahamu kila siku ili kupata mafanikio unayoyataraji.

Katika hatua yoyote unayopiga katika maisha yako kuwa tayari kutokukwepa changamoto kama kweli unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio. Changamoto utakutana nazo na zitakusumbua sana lakini kumbuka bado unao uwezo wa kukufanya kusonga mbele.

Sio kila mmoja utakuamini katika shughuli zako, unatakiwa kujiamini wewe 100% kwanza katika shughuli zako hata kama hujui uanzie wapi. Hata wasipo kuamini unakichwa ambacho ukikitumia vizuri kuna siku watakuamini.

Safari yako ya kutaka kufanikiwa utaanguka sana kabla ya kupata kile unachokitaka lakini hayo yote haimaanishi unatakiwa kuacha unachokifanya na kukipenda. Anguko lolote halinyofoi kichwa chako kwahiyo bado unasababu ya kusonga mbele ili ufanikiwe.

Sio kila mmoja ambaye atafurahishwa na hatua zako za mwanzo za kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa kwahiyo usitegemee kusifiwa na watu na kila mmoja. Hata kama hawatafurahishwa na unachokifanya kichwa chako ukikitumia vizuri hao ambao hawafurahi na ulichoanza nacho itawabidi wafurahishwe na shughuli zako.

Utakachoanza nacho wengi wanaweza kukiona hakipo sahihi lakini tambua wewe ni wewe na wewe ndiye unajua unachokifanya kwahiyo unatakiwa uthibitishe kwa kuweza kukifanikisha na sio kukiacha. Kichwa chako pekee ndicho chenye uwezo wa kufanya jambo lako kuwa sahihi kitumie ipasavyo.

Mafanikio ya mjasiriamali hayapimwi kwa umri, familia uliyotoka,kiwango au kwa kiwango cha pesa uliyonayo kuanza. Ukiamua kuthubutu,ukawa na nidhamu kwa unachokifanya, ukawa na juhudi mafanikio kwako hayataweza kupingika kwa baadae. Kichwa chako ni lulu na ndicho kipimo chako cha mafanikio.
Share To:

Post A Comment: