Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), inawafikisha watumishi wanne wa Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa tuhuma za rushwa na uhujumu uchumi.

Watuhumiwa hao ni; Deusdedith Katwale, Magori Matiku na Obadia Machupa ambao wote ni maafisa mazingira na Lydia Nyinondi ambaye ni Mhasibu Msaidizi. Wote wa makao makuu.

Taarifa iliyotolewa leo Juni 4 mwaka 2020 na Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani imesema, kuwa watuhumiwa hao, watasomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Share To:

Post A Comment: