Leo tarehe 29 Juni 2020, Mwanamuziki wa nyimbo za ukombozi Vitali Maembe amejiunga na ACT Wazalendo na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu katika Ofisi ya Chama Magomeni.

Akimkabidhi kadi ya uanachama, Ndugu Ado amemhakikishia Ndugu Maembe kuwa ACT Wazalendo litakuwa jukwaa sahihi kwake kuendeleza mapambano ya kudai haki, kupinga rushwa na kupigania umoja wa Afrika kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote kupitia sanaa.

Ndugu Maembe aliyewahi kuimba nyimbo ya "Sumu ya teja", "vuma" nk alitumia fursa hiyo pia kutangaza nia ya kugombea Ubunge kwenye Jimbo la Bagamoyo.

Janeth Rithe, Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma,

ACT Wazalendo.

29 Juni 2020.
Share To:

Post A Comment: