Tuesday, 16 June 2020

CCM WILAYA YA ILALA WAIPONGEZA MIRADI YA HALMASHAURI YA ILALA


NA HERI SHAABAN

CHAMA CHA MAPINDUZI  CCM Wilaya ya Ilala wameipongeza miradi ya maendeleo ya halmashauri ya Ilala   .

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma katika ziara ya Kamati ya Siasa Wilaya walipokuwa wakikagua miradi mbalimbali ya maendeleo 


"Nawapongeza halmashauri Mkurugenzi wa Ilala  na Watendaji wako tumekagua miradi yote mizuri   nawaomba watendaji mfanye kazi kwa weledi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala  ili kuakikisha Ilala yetu inasonga mbele"alisema Ubaya chuma..

Ubaya Chuma aliwataka Watendaji  kuwajibika kuwa Wazalendo kuunga mkono juhudi za Rais katika kusimamia miradi ya maendeleo ya serikali.


Aidha alipongeza Idara ya Elimu Msingi  Ilala kwa kufanya vizuri kila mwaka utekelezaji wa miradi yake shule.

Pia Mwenyekiti Ubaya Chuma ameipongeza Idara ya Mikopo ya halmashauri ya ILALA kwa utoaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Charangwa Selemani amewataka  Wenyeviti wa Serikali ya Mitaa wa  Wilaya ya Ilala kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu yao na kusimamia miradi ya maendeleo   wasiwe vikwazo kurudisha maendeleo nyuma.

"Nawaomba Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kwenda na kasi ya Rais wetu  John Magufuli katika kufanya kazi ili tujenge Tanzania ya uchumi wa viwanda "alisema Charangwa.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jumanne Shauri alisema Ilala wamejipanga vizuri idara zote  ikiwemo ukusanyaji wa mapato kila mwaka Ilala inafaya vizuri imepelekea miaka minne mfurulizo halmashauri hiyo inapata hati safi ya Mahesabu ya Serikali CAG.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment