Mwezeshaji wa Mradi kutoka Shirika lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida,  Witness Anderson (kushoto) akitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara wa Soko Kuu la Manispaa ya Singida ya namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mwezeshaji wa Mradi kutoka Shirika hilo,  Witness Anderson, akionesha namna ya kunawa mikono.
Afisa wa Shirika lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Geryson Janga (kushoto) akitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara wa Soko Kuu la Manispaa ya Singida ya namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona mkoani Singida leo.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona , Ipyana Mwakyusa akishirikiana na Shirika la SEMA, hapa anaonesha namna  sahihi ya kunawa mikono.
Elimu kwa njia ya mabango ikitolewa.
Afisa wa Shirika lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Gerson Janga (kushoto) akitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara wa Soko Kuu la Manispaa ya Singida ya namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona mkoani Singida leo.
Elimu kwa njia ya mabango ikitolewa. Kushoto ni Afisa kutoka SEMA, Mkasifu Daria John.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona , Ipyana Mwakyusa akishirikiana na Shirika la SEMA, hapa anaonesha namna  sahihi ya kunawa mikono.
Elimu kwa njia ya mabango ikitolewa.
Dotto Mwaibale na Boniface Jilili, Singida
SHIRIKA lisilokuwa la Serikali  Sustanable Environment Management Action  (SEMA) Mkoa wa Singida limetoa Elimu kwa Wananchi wa Mkoa huo juu ya namna ya kujikinga na Virusi vya Covid 19 vinavyo sababisha Ugonjwa wa Corona Shirika hilo linatoa Elimu hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Stromme East Africa Foundation lenye Makao Makuu Kampala nchini  Uganda huku ufadhili mkuu wa mashirika hayo ukitolewa na Shirika la Stromme Foundation la Norway kupitia Mradi wa uwezeshaji Jamii kiuchumi uliolenga vijana wakiume, wa kike, watoto na wakina mama.
Akizungumza wakati wa utoaji wa Elimu hiyo kwenye eneo la Soko Kuu la Manispaa ya Singida leo Ofisa Mradi kutoka Shirika la SEMA Renard Mwasambili amesema program wanayoitekeleza ni utoaji Elimu ya namna ya unawaji mikono, utoaji wa vifaa sambamba na elimu ya utengenezaji wa vifaa vya kujikinga na Virusi vya Covid 19 vinavyo sababisha Ugonjwa wa Corona.
"Lengo la Elimu hii ambayo tunaifanya ni kutembelea maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ya watu na kutoa elimu kwa mtu mmoja mmoja,makundi na wafanyabiashara namna ya kujikinga dhidi ya Ugonjwa huu."alisema Mwasambili.
Alisema kwamba program hiyo imewashirikisha pia maafisa wa EYP (Empower Youth Prosperity) kutoka Mkoani Mbeya na kuongeza kuwa Kila Mtanzania mahali alipo anapaswa kuchukua tahadhari na kamwe asipuuze ushauri wa kitaalamu unaoendelea kutolewa na Serikali pamoja na wataalamu wa afya.
Mwezeshaji wa Mradi kutoka Shirika hilo Witness Anderson alisema homa kali ya mapafu inayosababisha Virusi vya Corona ni Ugonjwa unaoambukizwa kwa kuingiawa na maji maji yatokayo kwenye njia ya hewa wakati mtu mwenye Ugonjwa huo anapokohoa ama kupiga chafya.
Alitaja njia nyingine ya maambukizi ni kwa kugusa maji maji yanayotoka puani (kamasi),kugusa kitambaa au nguo zilizotumiwa na mtu mwenye maambukizi ya Ugonjwa huo au maeneo mengine yaliyoguswa na mtu mwenye Virusi vya Corona.
Akielezea jinsi ya kujikinga na Ugonjwa huo alitoa tahadhari ya watu kukaa mbali angalau mita moja au mbili jambo litakalosaidia kujiepusha na maambukizi iwapo mmoja kati ya watu hao atakuwa na maambukizi.
Alisema tahadhari nyingine inayopaswa kuchukuliwa ni kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kutumia kitambaa safi au sehemu ya mbele ya kiwiko cha mkono,kuepuka kugusana na mtu mwenye dalili za Ugonjwa huo,kusalimiana kwa kushikana mikono,kukumbatia na kubusiana.
"Safisha mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka kwa kutumia sabuni au dawa ya kutakasa mikono na baada ya kunawa epuka kugusa macho,pua au mdomo na nguo badala yake jifute kwa kutumia tishu ambayo itatupwa sehemu salama baada ya kutumika."alisema Anderson.
Share To:

Post A Comment: