Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde amewataka watanzania kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa na watanzania na hasa Vijana ili kukuza soko la ndani na kuwawezesha kukua kimitaji.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa ziara fupi ya Kukagua na kujionea shughuli za uzalishaji zinazofanywa na Kampuni ya Vijana ya Platnum Paints iliyopo Mbezi,Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar ws salaam.

"Nawapongeza Vijana kwa hatua hii kubwa,Kampuni hii imetoa ajira kwa  zaidi ya Vijana 50 na mnaendelea kupanua shughuli zenu hivyo Vijana wengi watanufaika.

Niwaombe Watanzania tuunge mkono na kuthamini bidhaa zenye ubora zinazozalishwa ndani ya nchi ili kusaidia kuchochea ukuaji wa viwanda vidogo vidogo kwa sisi kuwa chanzo cha soko uhakika kwa Bidhaa zao.

Nimewaelekeza wataalamu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha Kampuni hii inasaidiwa kupata mkopo kupitia asilimia 4 ya Mapato ya ndani ili kuiwezesha kimtaji na kukuza shughuli zake"Alisema Mavunde

Akitoa maelezo ya Wilaya ya Kinondoni,Afisa Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi. Stella Msofe amewataka Vijana hao kutumia fursa ya kuomba mkopo kupitia asilimia 4 za mapato ya ndani na kwamba Wilaya ipo tayari kuwasaidia kufikia malengo yao.Wilaya ya Kinondoni imetenga zaidi ya Tsh bilioni 3kuwakopesha Vijana,Wakina mama na Wenye ulemavu katika mwaka wa fedha 2019/2020.

Akisoma Risala kwa ni niaba ya Vijana wengine wa Kampuni ya Platnum Paints,Bi. Arafa Maganga amebainisha kuwa vikwazo vikubwa vinavyiwazuia kukua kwa haraka ni ukosefu wa mtaji wa kutosha,dhana hasi juu ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi,upungufu wa vitendea Kazi na ufinyu wa eneo la uzalishaji.

Vijana hao wameomba kusaidiwa na serikali ili kuongeza uzalishaji zaidi na kuendana na falsafa ya serikali ya Dr John Pombe Magufuli ya Uchumi wa Viwanda.
Share To:

Post A Comment: