Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Daqqaro akisonyeshwa ramani ya alipotembelea ujenzi wa Tenki la maji Murriet wa kwanza ni Mkndarasi wa mradi huo,Mtaalam na Mashauri wa mradi,wa kwanza kulia ni Katibu tawala wa wilaya,Mkurugenzi Mtendaji AUWSA Mhandisi  Justine Rujomba
Daraja la kuvushia bomba River Crossing urefu wa mita 162 ambacho kipo Themi Njiro 
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akiteta jambo na Mhandisi mshauri wa mradi  kulia kwake ni Kimu Mkurugenzi mtendaji AUWSA Justine G.Rujomba Picha na Vero Ignatus
Mkuu wa Arusha Mjini Gabriel Daqqaro akionyeshwa  ramani kutoka kwa mkandarasi wa mradi katika eneo panapojengwa Tanki la maji ESAMI ambapo utakuwa unatoa lita milioni tatu Picha na Vero Ignatus 



Na.Vero Ignatus,Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro amefanya ziara ya katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira sambamba na kukagua ujenzi wa tanki la maji la Ngorbob,Olmot,mabwawa ya maji taka la Murriet,Kituo cha kusukuma maji (PS 5)Kivuko cha bomba ‘’Themi River Crossing ‘’ pamoja na kituo cha ulazaji wa mabomba kutoka (PS 2)  hadi Themi

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi Mhe.Daqqaro alitoa maagizo kwa  wahandisi na mhadisi mshauri kwamba eneo lenye mabwawa 18 ya maji taka likabidhiwe haraka kwa AUWSA ambapo ameiagiza Takukuru kufanya uchunguzi katika mabwawa hayo 18 ambapo mabwawa 8 kati yao yamebadilishwa ujenzi wao tofauti na ilivyokuwa awali bila kufuata utaratibu

Mhe.Daqqaro alimwagiza Kaimu Mkurugenzi mtendaji (AUWSA) Mhandisi Justine Rujoba kuunda tume ya wataalam ili kufuatilia kwanini mkandarasi alibadilisha uzanifu wa mabwawa kwa kuweka zege badala kuwa Kama ilivyoliwa awali amesema lengo la Serikali ni kutaka mradi huo ukawafaidishe vizazi na vizazi vijavyo kwani serikali Mara zote ni walinzi wa miradi hiyo na   kwa upande wa maji safi na maji taka kutoka asilimia 7.6%-30%

‘’Hata kama kwenda kwenye zege ni nzuri zaidi lakini kwanini utaratibu haukufuata wakati shughuli zote za serikali zinaendeswa kwa utaratibu na mawasiliano yanafanyika kwa maandishi ijulikane kwanini wamebadilisha kutoka mfumo wa awali na kwenda kwenye zege?alihoji Daqqaro

Aidha amemwagiza Mhandisi mshauri mradi kufanya kazi kwa maelezo ya serikali na wahakikishe kuwa wakati wanafukia mradi uwe na thamani halisi ya fedha kwasababu serikali imewekeza Zaidi ya milioni 41.2

Akizungumza Kaimu mkurugenzi mtendaji wa (AUWSA) Mhandisi Justine Rujomba amesema kuwa hadi sasa wameshajenga matenki 8 kati ya matenki 11 ambapo amesema mradi unaendelea vizuri ambapo wanatarajia kuzalisha maji lita milioni 24 kwa siku ambazo zitaongeza wingi wa maji mjini

Amesema katika mradi wa mabwawa wa maji taka wapo kwenye hatua ya mwisho wa ukamilishaji na mkandarasi karibia atakabidhi ila wamegundua kuna hitilafu ambazo watazifanyia kazi kabla mkandarasi hajakabidhi

‘’Tunaangalia hadi mwisho wa mwezi huu tutakuwa tumeshasafisha dosari zilizopo kama mkuu wa wilaya alivyotuagiza’’  alisema Rujomba

Rujomba alisema kuwa Mradi mkubwa kwa ujumla unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati  ambapo Kilimota 33 za bomba zimeshalazwa bado Kama kilometa 55 ambapo umegharimu jumla ya Bilioni 41.2

 Aidha tanki la maji  Olmot litakuwa linaujazo wa lita milioni mbili,Esami litakuwa na lita milioni tatu, Daraja la kuvushia bomba River Crossing urefu wa mita 162 ambapo utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na AUWSA kwa mkopo wa uliotolewa na Benki ya aendeleo ya Afrika ikishirikiana na Serikali ya Jamhurinya Muungano ya Tanzania Mradi huo umegawanyika katika vipengele kumi na mbili

Uchimbaji wa vuisima virefi 11 katika eneo la magereza seed Farm,nov 2017-june 2019,uligharimu USD 2,173,303.00,Ukarabati na upanuzi wa mtandao wa maji safi na maji taka katikati ya mji nov 2017-machi 2020 uligharimu USD 12,104,256.21,ujenzi wa mabwawa ya kutibu maji taka( WSP)Januari 2018-machi 2020 uligharimu USD 17,932,953.05,Uchimbaji wa visima 18MV na MM13-MM18 Julai 2018-Juni 2020,USD 4,195,928.00 uchimbaji unaendelea(3)na 3 uchimbaji upo katika hatua za maandalizi

Uchimbaji wa visima 6 (mm1-mm6)Julai 2018-juni 2020 USD 1,385,373.00,uchimbaji umekamilika,Uchimbaji wa visima 6(mm7-mm12)julai 2018-juni2020 itagharimu USD 1,383,074.00 uchimbaji umekalimika,Upanuzi wa mtandao wa maji taka nje ya CBD Agosti 2018-Agosti 2020 utagharimu USD 34,006,787.27 ambapo urefu wa bomba za maji taka trunk main 29.22km na lateral 38.38km jumla 67.60kmkati ya Zaidi ya 180.79.79km na mashimo ya ukaguzi 1196 katimya 4024 tayari yamejengwa ambapo imekamilika kwa 40.67%

Upanuzi wa mtandao wa majisafi ulianza oct 2018-Disemba 2020 umegharimu USD 110,419,202.45 ambapo kazi imekamilika kwa 33% ujenzi wa pumping station 4 kati ya 6 unaendelea ambapo ujenzi wa bomba kubwa za kusafirishia maji 58-843km zimelazwa kati ya 167.711km ambapo bomba za usambazaji wa maji safi 208km zimelazwa kati ya 380.380.375km, ujenzi wa ofisi kuu ya Mamlaka iianza octoba 2018 itagharimu TZS 7,476,366,485.00 kazi imekamilika kwa 12% ujenzi wa ofisi ya kanda ilianza okt2018-juni2020 imegharimu TZS 5,310,823.213 ambapo kazi imekamilika kwa 68.12%

Ujenzi wa mtambo wa kusafisha maji katika eneo la Midawe na kuboresha vyanzo vya maji vya olgilai na Sekei ulianza oktoba 2018-April 2020  umegharimu USD 3,073,250.04 ambapo kazi imekamilika kwa 75-22% na ujenzi wa vyoo vya mfano na elimu ya usafi wa mazingira ulianza nov 4,2019-nov 2020 utagharimu TZS 1,538,425,902.00 ujenzi wa vyoo 13 kati ya 25 unaendelea katika hatua mbalimbali na kazi hiyo imekamilika kwa 38%

MWISHO

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: