Tuesday, 5 May 2020

A TO Z IPO KWENYE HATUA ZA MWISHO KUTENGENEZA VAZI LA KITAALAMU KWA WATAALAM WA AFYA LINALOVALIWA WAKATI KUPAMBANA NA MAGONJWA MILIPOKU

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana akipokea barakoa 2000 kwa ajili ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha zilizotolewa na Kampuni ya A to Z ya mkoani hapa ikiwa ni kuendeleza Juhudi za Serikali kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Viongozi wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wakifuatilia hafla ya kupokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 iliyofanyika kwenye Ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo jijini Arusha

Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi za Jeshi la Polisi Magereza Uhamiaji Usalama wa Taifa kwenye hafla ya makabidhiano ya Barakoa 10,000 zilizotolewa na Kampuni ya A to Z kwa Serikali mkoa wa Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Kutoka kushoto ni Meneja wa kiwanda Cha A to Z Binesh Haria,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Joseph Massawe anayefuati ni Mkurugenzi Mtendaji mkuu wa Kiwanda Cha A to Z Shah Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pembeni yake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen wakiwa Meza kuu wakifuatilia Hafla hiyo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha


Meneja wa Kiwanda Cha A to Z akitoa Taarifa ya Vifaa vya barakoa 10,000 ambavyo wameikabidhi Serikali ya mkoa wa Arusha ikiwa ni mapambano ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 kutoka kwa Meneja Binesh na CEO wake Mr.Shah kwenye hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo Jijini hapa

Makabidhiano ya vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 yakiendelea leo jijini Arusha kwenye Ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen akipokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 kutoka kwa Meneja na CEO wa Kiwanda Cha A to Z leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
KIWANDA   cha kufuma Nguo Cha  A to Z cha jijini Arusha,kipo katika hatua za mwisho za kukamilisha utengenezaji wa  vazi maalumu linalotumiwa na wataalamu wa afya maarufu PPE,litakalovaliwa wakati wa  kuzikia watu watakaofariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona.

Hayo yameelezwa May 5 na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa AtoZ, Binesh Haria wakati akikabidhi msaada wa Barakowa  10,000,kwa mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.

Binesh,  amesema kiwanda hicho  tayari kimeshashona vazi hilo na limeshapelekwa  ngazi husika za serikali kwa ajili ya kuhakikiwa na mamlaka husika  na likipitishwa wataanza uzalishaji wake .

 Kuhusu msaada ,Binesh,amesema kiwanda hicho kimeamua kutoa mchango wake wa vifaa kinga vya korona kama sehemu ya kuunga mkono Jiji had a za serikali za kupambana na ugonjwa wa Corona. 

Akipokea msaada huo Mkuu  wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema  mtu  yoyote atakayekufa kwa Corona ndani ya Mkoa huo atazikwa kwenye makaburi yoyote  yaliyopo katika Mkoa huo huku familia zikipewa Uhuru wa kushiriki maziko hayo kwa heshima zote kwa watu wasiopungua 10 .

Amesema wataalam wa afya watatakiwa kufuata taratibu zote za afya ikiwemo kujiridhisha watakavyoona  inafaa na marehemu atasafirishwa ndani ya Mkoa wetu baada ya tahadhali zote kuchukuliwa.

Amesema endapo mgonjwa amekufa kwa Corona au hajafa kwa korona watu kumi tu ndio watakaomzika marehemu lengo ni kupunguza mikusanyiko makaburini.

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna alimshukuru Rc Gambo kwa juhudi kubwa za kutafuta vifaa kwa ajili ya kujilinda na ugonjwa huo kutumia wadau na pia alishukuru kwa mgao wa barakoa 2000 walizopatiwa. 

Katika mgawanyo huo Uhamiaji walipewa barakoa 500,CCM Mkoa barakoa 1,000 na Jeshi la Magereza barakoa 1,500 huku barakoa nyingine zikigaiwa katika tarafa mbalimbali za Mkoa wa Arusha. 

No comments:

Post a Comment