DR GODWIN.O.MOLLEL MBUNGE SIHA
NO. 0764594078
Kwanza nianze kwa kuipongeza serikali kwa jinsi inavyo pambana vizuri na tatizo hili la Corona,
Kupambana na ugonjwa Kama huu haina tofauti na kupigana vita ,na vita yoyote haitaji wasemaji wengi inaitaji wasemaji wa chache wenye ujuzi wa Kutosha kusemea vita, au wenyekusema baada ya ushauri wa Kutosha na kina kutoka kwa WATAALAMU waliobobea kupigana vita.
Na HATA Kama wewe ni mtaalamu wa vita ,Na siyo mamlaka ya kusema ,ukiwa unajambo unataka kushauri shauri kupitia mifumo halali ya WATAALAMU wa KIVITA ,
Ninaposhauri hivi simaanishi watu wasijadili wala wasiseme lolote la hasha na maanishi ,kabla ya kusema au kushauri angalia je ninachosema kimantiki kinaweza kuchanganya au kuleta taaruki au kifanye mifumo sahihi ya taarifa iyanze kutiliwa mashaka.
Mifumo sahihi ikitiliwa mashaka kwa uzembe wetu na UJUAJI wetu hakika hatawewe hutabaki salama, MIFUMO YA NCHI HII YA AFYA INAFANYA KAZI VIZURI SANA NA SHIRIKA LA AFYA DUNIA(WHO) PIA NA VYOMBO VIKUBWA VYA SCIENCE DUNIANI
JE WEWE NI NANI KUHOJI SANA NA KULETA TAARUKI ISIYO YA LAZIMA?
TUSIRUHUSU KAMWE MFUMO HALALI WA NCHI WAKUTOA TAARIFA UKAANZA KUTILIWA SHAKA, KWAAJILI YA MATAMKO YA BAADHI YETU YASIYOPIMWA ,MFUMO WETU UKIANZA KUTILIWA MASHAKA,
1.Mathara ni makubwa kwetu sisi humu na nchi ,kwani tutapoteza tumaini
2.Tutaufanya mfumo wetu upoteze kujiamini na ushusha uwezo kitendaji
USHAURI
1.Tupime sana ni yapi ya kusema mtandaoni na ni yapi ya kumpigia waziri au Wataamu wa wizara moja kwa moja
2.Tujue vita ikiwa vita siyo siasa tena ni science kazi yetu ni kumshauri mwenye mamlaka ili tushinde,
3.Tusiruhusu hawa ambao wanafanya kutoa ushauri publically tena wao si WATAALAMU ukiwatizama kwa jicho la tatu utaona tu nikama vile anatamani iwe mbaya ionekane alishauri alikuwa nabii akusikilizwa.
4.Tuwache kutoa matamko kwenye vyombo vya habari kwa kutumia hadidu rejea (fact) za mitaandao usiyo na hakika kuwa chanzo ni vyombo vya kisayansi halali(certified scientific document)
MSHANGAO KWANGU
1 .Ninashindwa kuelewa inakuwaje mbunge ambaye anakaa mita chache toka kiti cha waziri wa afya ,tena akiwa ndani ya bunge ,akiwa na dukuduku YEYE anaona tweeter ndio pakupeleka dukuduku.
2. Ivi tumesahau mbunge wewe ni mamlaka tosha wananchi wakisikia unawasiwasi ujarizika ,unadukuduku kimsingi wao wao watapoteza mwelekeo na kukata tamaa na HATA kinga ya mwili kushuka
3. Vita yoyote ni kwa vitendo na KUAKIKISHA saikologia (physicology) ya WATU wako na JESHI lako iko sawa,kutaaruki siyo suluhisho kwani tayari uko vitani ,ukipanic usipaniki vina iko palepale.
HITIMISHO
Matatizo MENGI ya afya duniani yametatulika kwa kutumia cultural sensitive approach (kutumia mbinu mwafaka kulingana na mila ,utamaduni imani na HATA uchumi wa eneo husika) na pia kwa kutumia WATAALAMU na watu walio fundishwa kupeleka ujumbe mahususi uliopimwa unaeleweka bila kuleta maana tofauti kwa JAMII husika.
ELEWA HATAMANENO HUPIMWA,KULINGANA NA MILA ,TAMADUNI,ELIMU,IMANI NA HATA UWEZO WA KIUCHUMI ,TUJIULIZE TUMETAMKA MANGAPI YASIYO PIMWA JE JAMII IMEPATA UJUMBE KAMA ULIVYOTEGEMEWA
JE NANI ATAPONYA TAARUKI?
TUUNGANE HII NI VITA SII JUKWAA LA KUTAFUTA MCHAWI
KUMBUKA GONJWA HILI LIMEPIGA WABABE WA SCIENCE WANYE SUPER COMPUTING SYSTEMS ZA VIRUS ,IMEPIGA JUMBA LA KIFALME ,
MKOMBOZI WETU NI MUNGU UMOJA WETU NA TAFAKURI YA KINA YENYE MISINGI YA SCIENCE KINA,NAUWEZO WA KUFIKIRI KATIKA HALI YA UTUPU(THINKING BEYOND THE BRAIN) NA UTUPU(ROHO) MUNGU NDIO MSINGI WAKE.
ASANTENI
Siyo msaafu ni tafakuri ya kibinadamu
Dr Godwin Mollel mbunge siha
Post A Comment: