NA PATRICIA KIMELEMETA

UGONJWA wa matundu kwenye moyo kwa watoto wachanga ni miongoni mwa magonjwa hatarishi ambayo yanaweza kusababisha udumavu au wakati mwingine kifo Kwa mtoto.

Ugonjwa huo ambao unaathiri kuta za ventrikali za moyo au kwa kitaalamu ujulikana kama (Ventricular Septal Defect) (VSD) unashambulia moyo wa mtoto jambo ambalo linaweza kumuongezea maradhi mengine.

Mtoto mwenye matatizo hayo,anaweza kubainika mara baada ya kufanyiwa vipimo ambapo kwa sasa hali inaonyesha kuwa, watoto wawili hadi 6 kati ya 1,000 wanaweza kuzaliwa na tatizo hilo.

Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania(MAT),Dk. Elisha Osati amesema kuwa, kutokana na hali hiyo, wazazi na walezi wana jukumu la kuwalinda watoto wenye natatizo hayo ili wasiweze kupata maradhi mengine ambayo yataweza kuhatarisha maisha yao.

"Taasisi ya Jakaya Kikwete imekua mstari wa mbele kuwasaidia na kuwafanyia operesheni watoto wanaozaliwa na matatizo ya moyo, lengo ni kuhakikisha wanapona kabisa ili waweze kukua vizuri," amesema Dk Osato.

Ameongeza kuwa, hivyo basi wazazi na walezi wana jukumu la kuhakikisha kuwa, wanawapeleka watoto wao hospitali mapema ili waweze kupatiwa matibabu pamoja na kuwalinda ili wasiweze kupata maradhi mengine ambayo yatahatarisha maisha yao.

Amesema kuwa, jukumu la ulinzi na usalama wa mtoto mwenye matatizo hayo linaanzia kwa mzazi au mlezi, hivyo basi wanapaswa kutimiza wajibu wao ili kuepuka changamoto za makuzi ya mtoto zinazoweza kujitokeza.

Amesema kuwa, serikali itaendelea kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa wazazi ili watoto waweze kukua vizuri ili wasiweze kupata matatizo mengine ambayo yatasababisha kudumaza ubongo wao na kushindwa kukua ipasavyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: