Mbunge  wa  Singida Magharibi,  Elibariki Kingu (wa tatu kushoto) akikabidhi moja ya bati kati ya 60 yenye thamani ya shilingi 1,300,000 ili kusaidia kupaua nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida katika hafla iliyofanyika juzi Viwanja vya Ofisi ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Alexandrina Katabi, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa huo, Alhaji Juma Kilimba, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Denis Nyiraha, Katibu Jumuiya ya Wazazi Mkoa, Mwalimu Ephraim Kolimba, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Singida Mjini, Ibrahim Mpwapwa na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Singida.
 Mbunge  wa  Singida Magharibi,  Elibariki Kingu, akizungumza wakati akikabidhi msaada huo.
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa huo, Alhaji Juma Kilimba, akizungumza wakati akipokea msaada huo.
 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Denis Nyiraha  akizungumza wakati wa kupokea msaada huo.
Nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida inayojengwa


Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE   wa  Singida Magharibi,  Elibariki Kingu amesaidia mabati 60 yenye thamani ya shilingi 1,300,000 ili kusaidia kupaua nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida. 

Elibariki Kingu alikabidhi msaada huo juzi  kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za umoja huo wa kujenga nyumba za makatibu wake ambapo pia alitoa seti moja ya Sofa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Katibu wa CCM mkoa huo.

"Kutokana na imani tuliyonayo sisi wabunge kwa chama chetu hatuachi kuweka mikono yetu kwenye shughuli mbalimbali za kichama."alisema kingu.

Akipokea vifaa hivyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaj Juma Kilimba alimpongeza Mbunge huyo kwani anaelewa kuwa kutoa ni moyo,pamoja na kuwa na mambo mengi kwenye jimbo lake lakini ameona kuna umuhimu wa kusaidia ndani ya chama hicho.

Alisema azma ya chama ni kuhakikisha kila mtendaji ndani ya jumuiya zote kwenye chama anajengewa nyumba ya kuishi ambapo wameanza na jumuiya ya umoja wa Vijana hivyo watakapo waomba tena kuchangia kwa ajili ya jumuiya zingine wafanye hivyo.

Aidha Mwenyekiti huyo alitoa rai kwa wafanyabiashara katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kutopandisha bei za bidhaa kwani Wizara husika imeshatoa maelekezo ya bei za bidhaa hususani sukari
"Waandishi tushirikiane katika kuwabaini wafanyabiashara ambao wanauza sukari na bidhaa zingine tofauti na maelekezo ya Serikari ili hatua zichukuliwe."alisema Kilimba.

Katika hatua nyingine Kilimba alitumia nafasi hiyo pia kuwaomba waandishi wa habari kwa kutumia fursa waliyonayo kusaidiana na viongozi wa chama na Serikali katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa wa Corona huku wakifuata maelekezo yote ya  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Denis Nyiraha pamoja na kupokea vifaa hivyo amemshukuru Mbunge huyo kwani wamekuwa wakipokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wabunge wa Mkoa wa Singida.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: