Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa wilaya  Arusha Gabriel  Daqarro ametoa siku saba kwa kaimu mhandisi  wa halmashauri ya jiji la Arusha Samwel mshuza    kuweka maji katika jengo la upasuaji  lililopo katika kituo cha afya  Cha Muriet ili kuanza shughuli za upasuaji.
 
Akizungumza katika siku ya pili ya ziara yake alipotembelea kituo hicho  katika kukagua ujenzi wa njia yakutembea kwa miguu inayounganisha majengo yote uliokamilika tarehe 4 March  mwaka huu wenye ghara a ya shilingi milion 100  .
 
Mkuu huyo amesema kuwa anatoa siku saba kwa mhandisi huyo kwani maji ni  sehemu kubwa ya kukwamisha  wananchi kupata huduma ya upasuaji pamoja na shughuli nyingine ndani ya majengo hayo.
 
Akiwa katika shule ya sekondari Taret mkuu huyo  amesema kuwa kabla ya mwaka wa fedha kuisha  majengo hayo  yawe tamekamilika  ili kuanza mwaka mwingine wa fedha isiokuwa na Madeni ya nyuma.
 
” Haitaleta maana nzuri kuona tunaanza  mwaka mwingine tukiwa na Madeni na kutokukamilisha  baadhi ya majengo tunatakiwa kuanza mwaka na miradi mingine sio ya viporo”. Alisema daqqaro
 
Hata hivyo mkurugenzi wa  jiji  Hilo Maulid Madeni amesema kuwa jiji limesimamisha shughuli zote za kawaida ili kuweza kukamilisha majengo yote .
 
” Mheshimiwa mkuu wa wilaya tunatambua wewe ni msaidizi wa Rais ndani ya eneo Hilo naomba nikuahidi jengo hili  ndani yasiku 30 litakuwa limekamilika”.
 
Akizungumza mmoja wa wananchi wa eneo Hilo Abdala maguta amesema kuwa wanaishukuru  serikali  kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kuwarahisishia wanafunzi wengi kutokwenda mashule ya mbali .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: