Tuesday, 17 March 2020

Waziri wa Kilimo Aahidi kushirikiana na TAHA

Waziri wa kilimo Mhe. Japhet Hasunga amehaidi kushirikiana na TAHA katika kuhimarisha na kukuza tasnia ya horticulture nchini.

Ameyasema hayo alipotembea ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini Arusha.
Akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Dkt.Jacqueline Mkindi amesema tasnia hiyo licha ya kutoa fursa kwa wananchi wengi na kuingizia kipato nchi, bado haitambuliki vyema.

Amemwelezea Mhe. Waziri kuwa TAHA anajitahidi kadri ya uwezo kuhakikisha tasnia hiyo inakuwa na hivyo kuinufaisha nchi kwa namna inavyo stahili.

Ameendelea kusema, dunia inafursa na pia bidhaa za nchi yetu zina nafasi ya kufanya vyema katika masoko ya ulaya, arabuni na amerika.

Akitolea mfano wa parachichi ambayo ina soko kwa sasa duniani, Dkt.Mkindi amesema soko la china, ulaya na amerika iko wazi kupokea bidhaa hiyo ambayo imethibitika kupendwa sana hasa inayozalishwa nchini mwetu.

Pamoja na hayo amemwomba Waziri kusaidia katika kuanzishwa kwa bodi/mamlaka ya kusimamia horticulture nchini.

Kwa upande wake Mhe.Hasunga amesema amejifunza TAHA na kwa sasa na mwono tofauti na alivyoijua taasisi hiyo.

Amesema vilevile kuwa tangu alipojua manufaa na ukubwa wa tasnia hiyo, wizara yake imeanzisha mikakati kadhaa ambayo itahakikisha tasnia hiyo inakwenda mbele.

Aidha Mhe.Waziri ameitaka TAHA kushirikiana na Serikali katika kutoa mwongozo na dira kama wazoefu katika tasnia katika kipindi hiki ambacho serikali inashughulikia uundwaji wa sera mpya ya kilimo.


No comments:

Post a Comment