Monday, 16 March 2020

WAZIRI NDALICHAKO KUZINDUA MASHINDAKO YA MAKISATU DODOMA, MSHINDI KULAMBA MILIONI TANO

 Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Maulilio Kipanyula akizungumza na washiriki na wadau wa ubunifu na teknolojia leo jijini Dodoma kuelekea wiki ya mashindano ya Teknolojia na Ubunifu yatakayozinduliwa kesho na Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako.
 Wadau na washiriki mbalimbali wa mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu wakimsikiliza Mkurugenzi wa Teknolojia na Ubunifu wa Wizara ya Elimu, Prof Maulilio Kipanyula wakati akielezea namna mashindano hayo yatakavyofanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia kesho.

Charles James, MsumbaTv
MASHINDANO ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) kwa mwaka 2020 yanatarajia kuanza kesho kwa muda wa wiki moja jijini Dodoma huku mgeni rasmi katika uzinduzi huo akiwa ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof Joyce Ndalichako.
U
Lengo la mashindano hayo ni kukuza ubunifu na kuongeza idadi ya watu wanaotumia vipaji vyao kubuni vifaa au vyombo mbalimbali kwa kutumia teknolojia.

Akizungumza na washiriki, wadau wa Makisatu na wandishi wa habari leo jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Prof Maulilio Kipanyula amesema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji ambavyo vipo mitaani na kuvisaidia kutimiza ndoto zao na kuisaidia Nchi yao.

Prof Kipanyula amesema mashindano hayo yanalenga kutambua wabunifu kutoka kwenye makundi saba na yatafanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa siku nne huku mshindi wa kwanza akijinyakulia kitita cha Sh Milioni Tano.

" Makundi hayo saba yatakayoshindana ni Shule za Msingi na Sekondari, Vyuo vya Ufundi Stadi, Vyuo vya Kati, Vyuo vya Kati, Vyuo Vikuu na Taasisi za Utafiti na Maendeleo na Ubunifu kutoka mfumo usio rasmi huku lengo kuu likiwa kuibua, kutambua na kuendelea ubunifu uliopo nchini.

Tupo hapa kuwanyanyua wote wenye ubunifu, ubunifu ni kujiongeza kwa kila jambo hivyo tunapobuni ni lazima tuangalie soko linataka nini siyo tunabuni vitu tunavyovipenda sisi hapana! Ni lazima tuzingatie uhitaji wa soko," Amesema Prof Kipanyula

Ameongeza kuwa kuelekea uchumi wa kati ambao unategemea viwanda suala la ubunifu ni la umuhimu na kwamba kwa wale wote wenye utaalamu na ubunifu ndio watakaopata fursa zilizopo nchini kwa sasa.

" Niwapongeze washiriki wote niwaambie ukweli, ubunifu ni utajiri mkubwa sana. Na sisi kama Wizara tutaendelea hakika kushirikiana na nyie na kuwapa sapoti yetu kwa kadri itakavyowezekana," Amesema Prof Kipanyula.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilianzisha mashindano hayo mwaka  jana lakini mwaka huu wameamua kushirikiana na wizara nyingine ikiwemo Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambayo itasimamia uratibu, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTEC) pamoja na VETA huku kauli mbiu ikiwa ni "Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa uchumi wa viwanda".

Prof Kipanyula amesema mashindano hayo kwa yamekuwa na manufaa makubwa kwani kutokana na mashindano yaliyofanyika mwaka jana waliweza kuibuka washindi 60 ambapo wameendelezwa na kwa sasa wanajipatia kipato kutokana na ubunifu wao.

Katika mashindano ya mwaka huu mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha Sh Milioni Tano na tuzo, mshindi wa pili atazawadiwa kiasi cha Sh Milioni Tatu na mshindi wa tatu akipata Sh Milioni mbili.

 Katika mashindano haya atapata kitita cha Sh Milioni Tano na tuzo, mshindi wa pili atazawadiwa kiasi cha Sh Milioni Tatu na mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha Sh Milioni mbili," Amesema Sylvia

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeamua kuanzisha mashindano yatakayoibua vipaji mbalimbali.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma, Mkurugenzi 
Amesema makundi saba yatakayoshiriki mashindano hayo ni Shule za Msingi, Shule za Sekondari, Vyuo vya Ufundi Stadi, Vyuo vya Kati ,Vyuo Vikuu, Taasisi za utafiti  na maendeleo na wabunifu kutoka mfumo usio rasmi huku lengo kuu likiwa ni kuibua,kutambua na kuendeleza ubunifu.

Hivyo niwaombe ndugu zetu wanahabari kuweza kuwahabarisha wananchi wetu kujitokeza kwa wingi kuanzia Machine 16 hadi 20 mwaka huu katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma waweze kupata fursa ya kuonesha vipaji vyao," Amesema Prof Kipanyula.

Nae Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka Wizara ya Elimu, Sylvia Lupembe amesema kuwa  kwa mwaka huu washiriki wabunifu waliojitokeza kushiriki mashindano hao ni 583  na zoezi lilishafungwa huku tathimini ikiendelea kufanyika huku pia taasisi 61 zikithibitisha kushiriki

No comments:

Post a comment