Tuesday, 10 March 2020

WANANCHI RUJEWA WAKIMBIA MAKAZI YAO KWA MAFURIKO ...

Wananchi wakikimbia makazi yao kwa mafuriko 


Na Oliver Motto Mbarali

Ni hali tete katika vitongoji mbalimbali kikiwemo kitongoji cha Magea, Ihanga na Jangurutu -vilivyopo katika Kata ya Rujewa Wilayani Mbarali mkoani Mbeya kufuatia mafuriko yaliyowakumba .

Kutokana na mafuriko hayo maji ya mvua yameingia katika makazi ya watu na kusababisha taharuki, na hiyo ni baada ya mvua kubwa kunyesha na kujaza mto Mbarali.

Zabibu Nuroo na     Halima Abdul, wakazi wa Rujewa  wamesema maji hayo ni hatari kwa usalama wao, kwani yanakwenda katika makazi yao kwa kasi, jambo ambalo ni hatari zaidi kwa watoto na wazee wasio na uwezo wakujinasua nayo.

Aidha Zabibu amesema endapo kingo za mto huo hazitaimarishwa, kuna hatari zaidi kwa wakazi wote wa Rujewa, kwakuwa maji yote ya mto Mbarali yataingia katika makazi ya mji huo wa Rujewa na kusababisha maafa makubwa, jambo linalowezakuepukika kwa kurejesha maji katika mkondo wake wa awali kwa kuziimarisha kingo za mto huo ambazo zinavunjika kila mvua zinaponyesha na maaji kuongezeka.

Zuhura Lutumo na Shani Bumbo, wakazi wa Magea Rujewa,  wanasema ni vyema kuyakimbia makazi ili kuokoa uhai wao– ingawa wapo wanaoona hasara itawakumba mara baada ya muziacha mali zao.

Salekh Hussein ameamua kumchukua mbwa wake kama sehemu ya mali yake, kwa madai kuwa ndiyo mali yake anayoipenda.

Rubern Mfune Mkuu wa Wilaya ya Mbarali anatoa wito kwa wananchi, akiwasihi kuhama mara moja katika mazingira hatarishi ili kunusuru uhai wao.

No comments:

Post a comment