Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo katika Wilaya ya Morogoro, ambalo linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu.
 Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo katika Wilaya ya Morogoro (kulia) linalotarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu  na (kushoto) ni jengo linalotumika  sasa na  mahakama hiyo.
 Wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria  wakitoka kukagua leo  jengo la sasa la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.
 Wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria  wakiingia  kukagua leo  jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria, Mhe. Emmanuel Mwakasala  na (wa tatu kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga, wa (kwanza kushoto) ni  Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa   Majengo  ya Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni  Mchome wakikagua leo  jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja  leo na Wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria mara baada ya wajumbe hao kutembelea jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro. Wengine ni baadhi  ya viongozi wa Mahakama ya  Tanzania. (Picha na Magreth  Kinabo – Mahakama)
Share To:

Post A Comment: