Na Woinde Shizza,KILIMANJARO

WAFANYABIASHARA 10  wanaomiliki maduka katika eneo la stendi kubwa Moshi mkoani Kilimanjaro wamelazimika kuvunja kufuli mara baada ya kufungiwa maduka yao   na mgambo wa Manispaa kwa madai kwamba sio wapangaji halali

Wakizungumzia tukio hilo kwa niaba ya wafanyabiashara hao Iren Charles ameleza kwamba wananyanyasika na Mgambo wa Manispaa ya Moshi kwa  kuwavamia na kufunga maduka yao hivyo kukazimika kuvunja kufuli hizo.

Ameeleza kuwa  walifungua kesi Mahakamani ya kupinga kufungiwa maduka yao  na Mahakama kuwaruhusu kuendelea na biashara kama kawaida lakini mgambo wamekua wakifika katika maduka yao na kulazimisha kufunga kwa nguvu .

Ameongeza wao  ni wamemiliki maduka hayo kwa muda mrefu wa  zaidi ya miaka 15  huku wakilipa kodi zote na kutambulika na Manispaa ya Moshi lakini sasa kilichotokea ni madalali kuingilia kukodisha maduka yao kwa garama kubwa sana.

Amesema madalali ndio chanzo cha wao kukosa maduka hayo kwani zabuni ilipotangazwa ilikua ni kubwa yenye lengo la kuwakwamisha kibiashara kwa  kuwataka kulipa kiasi cha shilingi 300,000  kwa mwezi jambo ambalo hawawezi kulipa garama hiyo

Wafanyabiashara hao wameomba viongozi wa Serikali kuingilia kati kwani wananyanyasika kufungiwa maduka yao huku wao ni wazawa wanaitaji kulipa Kodi na kuleta maendeleo katika manispaa yao

Akijibu maelezo ya wafanyabiashara hao Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Maiko Mwandezi anasema ni kweli walikua na mikataba na wafanyabiashara hao lakini ilisha na walitangaza zabuni  kwa mujibu wa sheria na zabuni ilivyopita hawakushinda na kutakiwa kukabidhi maduka hayo.

Amesema wafanyabiashara wanacho kifanya ni kuleta vurugu tu kwani mpaka sasa wamesha vunja makofuli zaidi ya 70 katika maduka walioweka zuio la kutoingia na kutaka kukabidhi maduka kwa walioshinda tenda ambao ni wapangaji wapya

Kuhusu kutambua zuiyo lilotolewa na Mahakamani, Mkurugenzi amesema kwamba wanalitambua na wafanya Biashara walipaswa kufunga maduka mpaka hapo kesi ya msingi itakapo kwisha Mahakamani lakini wameendelea kufanya biashara bila kua na mikataba jambo ambalo ni kinyume na sheria

Hata ivyo Mkurugenzi amedai kuwaburuza Mahakamani wafanya biashara hao wapatao 10 kwani kati ya wafanya biashara wapatao 130 hao 10 ndio wanao sumbua Serikali kwa kuikosesha mapato kwa muda wote walio pewa barua za kuondoka na kuachia maduka hayo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: