Sunday, 8 March 2020

UONGOZI CUF WAIGEUKIA ZEC ....

Chama Cha Wananchi (CUF) kupitia baraza kuu la Uongozi Taifa limeiomba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuwaandikisha wananchi weye sifa katika daftari jipya la wapiga kura bila ya ubaguzi ili kuwa na orodha ya wapiga kura ambayo ni halali.

Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa CUF Taifa , Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipokuwa akitoa ripoti ya baraza kuu la uongozi Taifa ya kikao chake cha kawaida kilichofanyika Machi 5 hadi 6 mwaka huu.

Amesema hatua hiyo imekuja baada ya Baraza kuu la Uongozi Taifa kusitushwa na kusikitishwa na uandikishaji mdogo wa wapiga kura Zanzibar.

" Kimsingi ZEC inaandikisha daftari jipya la wapigakura ambao wanapaswa kuwa na kitambulisho kipya Cha ukaazi_  Zan _ID mpya na wazazibar wengi tunaona hawajaoewa Zan-ID na kwa hiyo wamenyimwa haki ya kujiandikishwa kuwa wabiga kura"amesema Profesa Lipumba

Ameongeza kuwa, wananchi wengi wenye sifa ya kuandikishwa kuwa wapiga kura wamenyimwa fursa hiyo baada ya kunyimwa vitambulisho vya ukaazi kwa sababu za kisiasa.

Akitolea mfano Profesa Lipumba,  amesema idadi ya wapigakura waliondikishwa katika Jimbo la konde ni 4,331 ukilinganisha na idadi ya wapigakura kura 9299 waliondikishwa katika Uchaguzi wa mwaka 2015.

Amesema kwa upande wa jimbo la Wete lilikuwa na wapiga kura waliondikishwa 8574 kwa mwaka 2015 lakini hadi kufikia Sasa waliondikishwa ni 3597.

"Mwalimu Nyerere alieleza haki ndiyo msingi wa imani na kunyimwa wazazibari haki ya kupiga na kuchagua Rais , Wawakilishi, Wabunge na madiwani ni kuvunja msingi wa amani "amesema Profesa Lipumba

Aidha amewataka wananchi wa Zanzibar kuhamasisha na kujitokeza kwa wingi kudai haki yao kujiandikishwa katika daftari la wapiga kura ambalo linaendelea hivi sasa visiwani humo ili kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi .

Pia Profesa Lipumba ameiagiza kamati ya utendaji ya Taifa kuhamasisha Mchakato wa kutoa kalenda ya Mchakato wa uchukuaji na urejeshaji was fomu kwa wanachama watia nia wa wanafasi za udiwani ,ubunge na Urais.

Katika hatua nyingine Profeda Lipumba amesema baraza hilo limempogeza kutoka na kuhamasisha wananchi katika ziara yake ya hivi karibuni kuendelea na kazi ya ujenzi wa Chama kwa kuiamarisha matawi.

Pia baraza hilo limeiomba Serikali kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hasa WHO kuandaa mkakati madhubuti wa kukabilina na mlipuko wa virusi vya Corona 19 .

" Benki ya Duniani, Shirika la fedha la Kimataifa na benki ya maendeleo ya Afrika limetagaza kuwepo kwa mifuko ya dharura ya kukabilina na ugonjwa wa virusi vya Corona "amesema Profesa Lipumba.

No comments:

Post a comment