Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) wakiwa kwenye mafunzo maalu juu ya kupambana na kuzuia ugonjwa wa virusi vya Corona mapema leo Machi18 Jijini Dar es Salaam.

Afisa Majaribio na Usalama wa dawa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Dkt. Alex Nkyamba (kulia) akitoa mafunzo hayo
.........................


MAMLAKA ya dawa na Vifaa tiba (TMDA) imewapatia mafunzo maalum watumishi wake ya kupambana na kuzuia ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona COVID 19   ulioikumba dunia kwa sasa.

Mafunzo hayo maalum yametolewa na Afisa Majaribio na Usalama wa dawa wa Mamlaka hiyo, Dkt. Alex Nkayamba katika ofisi za TMDA zilizopo Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Katika mafunzo hayo watumishi hao kutoka idara mbalimbali za Mamlaka hiyo waliweza kupokea mafunzo ambapo pia watakuwa mfano na walimu kwa wengine katika maeneo ya kazi na nyumbani

Hadi sasa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza uwapo wa visa vitatu vya wagonjwa wa  Corona.

Ugonjwa huo umekuwa ukienea kwa kasi karibu nchi mbalimbali duniani ambapo tayari mamlaka zimewataka wananchi kuchukua hatua mahsusi za  kujikinga na kuondoa hofu.

Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuziba mdomo wakati wa kukohoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara ama kwa vitakasa mikono (hand sanitizer) pamoja na kuepuka sehemu zenye mikusanyiko ya watu.

TMDA imeweka mifumo mbalimbali  katika udhibiti wa ubora, usalama na unafanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya za jamii.

Huduma za TMDA hutolewa kwa kuzingatia viwango vya mkataba wa huduma kwa wateja wa mwaka 2016.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: