Tuesday, 3 March 2020

RC HAPI AVUTIWA NA MATUMIZI YA FEDHA ZA EP4R MANISPAA YA IRINGA ,ATOA AGIZO KUANZISHA BENKI YA TOFALI

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akikagua ujenzi wa sekondari ya Igumbilo 

Mkuu wa mkoa wa Iringa akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa fedha za EP4R  Manispaa ya Iringa
.....................................

MKUU wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amepongeza usimamizi  wa fedha za lipa kulingana na matokeo (EP4R) Manispaa ya Iringa huku  ameagiza viongozi wa vijiji na mitaa katika mkoa huo kusimamia uanzishwaji wa benki za tofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu .

Akitoa agizo hilo jana baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili  katika shule ya Msingi Nyumbatatu na Ujenzi wa nyumba ya mwalimu na vyumba vya madarasa shule ya msingi Hoho .

Hapi alisema kuwa kutokana na uchakavu wa majengo mengi ya shule za msingi na nyumba za walimu katika mkoa wa Iringa kuna haja ya kuweka mkakati wa kuanzisha benki za tofali ili kuendelea kuboresha vyumba vya madarasa na nyumba za walimu .

Hivyo aliagiza viongozi kuhimiza na kusimamia wananchi kufyatua tofali za kutosha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi katika shule mbali mbali ambazo hali yake si nzuri .

"Niendelee kusisitiza kila mtaa ,lila kijiji na kila kata kuwa na benki ya tofali ili kuwezesha ujenzi wa majengo mbali mbali pindi yanapohitajika "

Alisema kuwa pale inapotokea kuna upungufu wa vyumba vya madarasa ni rahisi kuanza ujenzi maana wajibu wa serikali kutoa bati ,saruji na ujenzi .

Pia aliagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kufanya mchakato wa kuandaa andika kwa ajili ya kuziombea pesa shule chakavu zote ili kuweza kuzifanyia uboreshaji maana hali ya shule hasa zile za miaka 1960 na kuendelea ni mbaya sana zinahitaji pesa nyingi ili kuziboresha zaidi.

Alisema kuwa kwenye andiko ambalo Halmashauri italiandika kwenda wizara ya elimu kuelezea hali ya uchakavu wa majengo ya shule ni vema kuambatana na picha za majengo hayo ili serikali iweze kuona na kutoa fedha za uboreshaji .

Kwani alisema uwezekano wa serikali kutoa fedha hizo ni mkubwa na kuna shule ya msingi katika wilaya ya Mufindi imepewa zaidi ya shilingi milioni 641 kwa ajili ya ukarabati wa shule  .

Kuwa huwezi kupata fedha serikalini pasipo kufikisha maombi kupitia andiko ambalo litaonesha uhalisia wa majengo .

Katika hatua nyingine Hapi alipongeza usimamizi mzuri wa fedha za lipa kulingana na matokeo (EP4R) kwani zimeweza kufanya kazi nzuri na kubwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa baada ya kujenga majengo yenye kiwango kwa gharama ndogo .

Awali mkuu wa shule ya msingi Hoho Wambura Kimoko alisema kuwa kupitia fedha za EP4R Katika shule hiyo kwa mwaka 2019 walipokea kiasi cha shilingi milioni 25 zilipokelewa kwa ajili ya umaliziaji wa boma moja na kukarabati nyumba moja ya mwalimu .

Kuwa kwa ajili ya umaliziaji wa vyumba vya darasa na kukarabati nyumba moja ya mwalimu .

Alisema katika fedha hizo   shilingi milioni 22 .5 zikitumika kumalizia nyumba na vya madarasa na nyumba ya mwalimu kiasi 12.5 kukarabati nyumba ya mwalimu .

Pia alisema pamoja na fedha kiasi cha shilingi milioni 25 kutolewa na serikali kuu pia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia makusanyo yake ya ndani imechangia fedha kwa ajili ya uboreshaji wa shule hiyo .

No comments:

Post a comment