.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikongosi wilaya ya Mufindi jioni ya leo .

Na Francis Godwin, Mufindi
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amekataa ha Ikongosi wilaya ya Mufindi la kuomba ardhi ya kulima katika eneo la jeshi la magereza .

Hapi alikataa ombi hilo Leo wakati wa mkutano wake wa kupokea kero za wananchi wa wilaya ya Mufindi .


Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa ardhi ya magereza ni kwa ajili ya matumizi ya magereza kuzalisha chakula kwa ajili ya wafungwa.

Hivyo alisema kuwa sio kila ombi la wananchi anatakiwa kuwatekelezea kwani kimsingi ardhi ya magereza ni maalum kwa ajili ya utaratibu wa serikali kuhifadhi ardhi yake kwa ajili ya matumizi yake ya baadae.

"Serikali ina kawaida ya kuwekeza benki ya Ardhi kwa ajili ya matumizi ya kijamii ikija kutokea wananchi wameongezeka na serikali inahitaji kujenga kituo cha afya ama shule benki yake ya ardhi ni kwenye ardhi hiyo iliyowekezwa kwenye taasisi zake kama magereza,jeshi la kujenga Taifa na maeneo mengine"

Kwani alisema Kama wananchi wataruhusiwa kulima kwenye ardhi hiyo iliyohifadhiwa itakuwa ngumu kwa baadae kuja kuichukua ardhi hiyo kwa matumizi ya umma.

Aidha alisema iwapo wananchi wanahitaji eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule wanaweza kukaa chini na Magereza ili kupewa eneo Ila sio kwa ajili ya kilimo .

Kwani alisema kimsingi shule ni mali ya serikali na magereza ipo chini ya serikali hivyo wanaweza kupewa eneo la ujenzi na kuwekewa mipaka.

"Ila niwaeleze wazi wananchi kuwa sio kila ombi mnaloomba mnaweza kusikilizwa maombi mengine hayawezekani kama hili la kuomba ardhi ya magereza kwa ajili ya kulima  watu binafsi "

Hata hivyo Hapi aliagiza magereza kutumia wafungwa kuendeleza ardhi hiyo kwa kilimo Kama Rais Dkt John Magufuli alivyoagiza kwa magereza zote nchini kutumia wafungwa kuzalisha chakula Chao wenyewe .

Kuhusu mashamba ya bega kwa bega (Ujamaa) yaliyotolewa enzi za utawala wa serikali ya awamu ya kwanza kukaa chini viongozi wa kijiji ili kuona sehemu ya ardhi iliyobaki kutenga kwa ajili ya malisho  ya mifugo Kama ambavyo wananchi wanavyoomba.

Kwani alisema malalamiko ya wananchi hao kulalamikia ardhi hiyo ambayo waligawa wenyewe kwa taasisi za dini.

Katika hatua nyingine mkuu huyo  wa mkoa aliwataka wananchi wenye malalamiko juu ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)na wana namba za NIDA  kuendelea kutumia namba hizo kusajili laini zao za simu pia kuendelea kutumia vitambulisho vya mpiga kura.

Mkuu wa magereza la (SP) Isupilo Benjamin Kabisa  alisema wamejipanga kulinda ardhi ya magereza pamoja na kutekeleza agizo la Rais la kuagiza magereza kuzalisha chakula kupitia wafungwa
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: