Na Frankius Cleophace MsumbaTv Tarime.

Mwanamke mmoja aliyefaamika kwa jina la Rhoda James mwenye umri wa miaka 25  mkazi wa kijiji cha Turugeti Kata ya Bumera Wilayani Tarime Mkoani Mara amefukukuzwa nyumbani kwake akiwa na mtoto mdogo wa siku sita pamoja na watoto wake wane.

 Mwanamke huyo amedai kuwa mme wake anayejulikana kwa jina la Chacha Mwita mkazi wa Turugeti kata ya Bumera   amemfukuza baada ya kushawishiwa na Mama mkwe wake kuwa hatakiwi katika familia hiyo.

“Mama mkwe kila asbuhi anakuja nyumbani anakuta bado tumelala na mme wangu anafungua mlango na pazia anatoa mabegi yangu na kutupa nje huku akimwambia kijana wake kuwa anifukuzwe la sivyo atampa laana” alisema Rhoda.

Rhoda alisema kuwa kipindi anakaa Mjini kabla ya kwenda kijijini kwa kipindi cha miaka Minne hapakuwepo na changamoto yeyote kwa Mme wake lakini baada ya kwenda kijijini tangu Desemba 2019 ndipo Matatizo yameanza tukiwa kijijini huku akidai kuwa yeye ni mke wa pili kwa mme wake.

Pia Mwanamke huyo aliongeza kuwa  amefukuzwa pamoja na watoto wake wadogo ambapo mtoto wa kwanza   ana umri wa Miaka 08, Wa pili Miaka 05,watatu 04 wa Nne Miaka 03 na wa tano ni mtoto mdogo ambaye amezaliwa hivi karibuni ana siku sita tu

“Mfano kama mtoto huyu mdogo mpaka sasa hana nguo na mvua zinanyesha kuna baridi anaweza kuugua nimenyanyaswa sana pia kujifungua nilijifungulia kwa majirani hivyo naomba serikali iweze kunisaidia ili nilee watoto wangu wote ni wadogo pia wazazi wangu walishakufa” alisema Mwanamke huyo.

 Vilevile Rhoda alisema kuwa watu wenye mapenzi mema wamejitokeza na kuchanga nauli baada ya kufukuzwa na ndipo alilazimika kuja mjini kwa ajili ya kuomba msaada lakini watoto wake wanachangamoto kubwa.

Kutokana na changamoto hiyo ya utengano wa familia wenda watoto hao wasipate haki yao ya kupata elimu, malezi bora ya wazazi wawili licha ya serikali pamoja na mashirika kuendelea kupaza sauti kuhusu haki za watoto sasa serikali iweze kuingilia kati kwa lengo la kusaidia watoto hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mara Samwel Kiboye  amelaani vikali kitendo hicho huku akiomba jeshi la polisi kumsaka Mme pamoja na Mama mkwe  ili wachukuliwe hatua kali  dhidi ya ukatili huo.

“Nimepigiwa simu kuhusu tukio la mama huyo nimefika ni suala la kusikitisha nimetoa fedha ili mama huyo apate sehemu ya kulala pia  watoto wapate chakula na mtoto huyu mdogo anunuliwe nguo ili kesho polisi waendelee na taratibu lazima sisi viongozi tuwasaidie wananchi wanaokumbwa bna ukatili wa kijinsia alisema Kiboye

Suala la Malezi na Makuzi ni jukumu la wazazi wawili kwa maana Baba na Mama hivyo jamii haina budi kuondokana na suala la ukatili dhidi ya Mama na mtoto.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: