Tuesday, 24 March 2020

MSALABA MWEKUNDU WATOA VIFAA KINGA KUKABILIANA COVID 19

Viongozi wa shirika la msalaba mwekundu Jiji la Arusha akitoa msaada wa vifaa vya Usafi wa maji ya kutiririka ambavyo vitawekwa kwenye maeneo ya Stand kuu ya Mabasi na vituo vya daladala sanjari na masoko kwa Afisa Tarafa ya Themi leo jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Afisa wa shirika la msalaba mwekundu akionyesha sehemu ya vifaa hivyo ambavyo amekabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Arusha leo
Shirika la msalaba Mwekundu limetoa vifaa vya kunawa mikono ikiwa ni kuongeza Juhudi za kupambana na Ugonjwa wa Covid 19 au virusi vya Corona ndani ya jamii mkoa wa Arusha.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo leo jijini Arusha kwa mkuu wa wilaya hiyo Gabriel Daqarro wakati huu ambao Serikali imeendelea na mapambano ya Ugonjwa wa Covid 19.

Suala hilo limekuja wakati tangia kisa cha kwanza Cha mgonjwa wa Covid 19 kutangazwa nchini huku Serikali ukiendelea kutoa elimu ya kusaidia kutokuwa na maambukizi mapya hapa nchini.

Hadi Sasa hapa nchini kumekuwa na wagonjwa 12 tangia Serikali kutangaza kisa Cha kwanza mkoani hapa hali ambayo imefanya mh.rais kuwataka watanzania kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wakifuata maelekezo mbalimbali ya Serikali kuendelea kuudhibiti Ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment