Tuesday, 24 March 2020

Mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite Arusha ashikiliwa na vyombo vya dola


2346505_Mulla20Masai20Nssf2020190807_153839.jpegMfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha na Manyara, Mulla Oleshangiki anashikiliwa na vyombo vya dola kwa takribani wiki mbili mpaka sasa.

Mfanyabiashara huyo alishikiliwa jijini Arusha na vyombo vya dola baada ya taarifa kudai kwamba amekuwa akijihusisha na biashara hiyo ya madini huku akikwepa kulipa kodi serikalini.

Mfanyabiashara huyo ambaye amekuwa na urafiki wa karibu na baadhi ya vigogo wa serikali mkoani Arusha alishikiliwa wiki iliyopita na kisha kwenda kupekuliwa nyumbani kwake ambapo alikutwa na baadhi ya madini ya Vito ambayo hayajalipiwa kodi Serikalini.

Mara baada ya kupekuliwa alifikishwa katika kituo cha polisi kitengo cha Utalii na kisha kuhifadhiwa hapo kabla ya kuchukuliwa na task force na kisha kupelekwa jijini Dar es salaam kwa mahojiano zaidi.

Mulla amekuwa akifadhili Kwaya mbalimbali za dini mkoani Arusha lakini pia amekuwa miongoni mwa wafadhili wa klabu ya Gwambina FC inayomilikiwa na mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti.

Pia ni Miongoni mwa wadau wa maendeleo katika mkoa wa Manyara ambapo amefadhili ujenzi wa shule na visima vya maji.. Pichani ni mfanyabiashara

No comments:

Post a Comment