Monday, 16 March 2020

MATUKIO YA MGONJWA WA VIRUSI VYA CORONA AU COVID 19 JIJINI ARUSHA KABLA YA KUPELEKWA ENEO LILILOTENGWA NA SERIALI

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha akiwa kwenye ufuatiliaji wa  maandalizi ya sehemu ya kumuweka mgonjwa wa kwanza wa Corona baada ya kutangaza leo na wizara ya Afya kwenye hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.

Hali halisi Mara baada ya taarifa ya kisa Cha kwanza Cha mgonjwa wa virusi vya Covid 19au Corona virus baada ya kutangazwa na Waziri mwenye dhamana na Afya Ummy Mwalim kwenye hospitali ya Mount Meru akitokea nje ya nchi nchini Ubelgiji.

Maandalizi ya kwenda kumchukuwa mgonjwa huyo na kumpeleka sehemu iliyotengwa na serekali yakiendelea.

Msafara wa kwenda kumchukuwa mgonjwa huyo maeneo ya uzunguni ukiondoka kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru jijini Arusha

Hotel aliofikia Mtanzania huyo jijini Arusha ikiwa imefungwa huku watu wote wakizuiwa kuingia au kutoka ndani ya hotel hiyo hapo Kamanda akiondoa Utepe kuruhusu gari la wagonjwa kuingia kumchukuwa mgonjwa huyo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akivaa kifaa maalumu Cha kujizuia kupata maambukizi yavirusi vya Covid 19 au Corona virusi kabla ya kusimamia zoezi la kuhakikisha mgonjwa huyo anapelekwa kwenye eneo lililotengwa na serikali

Gari la wagonjwa likiingia kwenye hotel iliyopo eneo la uzunguni karibu na hotel ya pepe ambapo ndipo mgonjwa huyo alifikia picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa na kamati ya ulinzi wakiwa kwenye hotel aliofikia Mgonjwa huyo jijini Arusha picha zote Ahmed Mahmoud Arusha
Hofu kubwa ya wananchi juu ya ugonjwa wa Covid 19 bado inaohitajika elimu kwao kwani imeonekana bado wengine wamekuwa wakijiziba na magazeti au makaratasi kukwepa maambukizi ya virusi vya Covid 19 au Corona

Hali hiyo imetokana kisa Cha kwanza kuripotiwa Cha kugunduliwa kwa mgonjwa wa Covid 19 au Corona aliyeingia Jana kupitia uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

Pamoja na suala hilo limekuwa na wananchi ambao wanahitaji elimu kwani wengi wao walitembelea ndugu zao wagonjwa wamekuwa wakitembelea akijifunika magazeti wengine nguo zao baada ya kupewa taarifa hizo.

Pia juhudi za.serikali zinahitaji kwa haraka kuweka dawa na vifaa kwa wananchi na wagonjwa wanaokuja kupata huduma hospitalini hapa ikiwemo barakoa za kujizuia kutokana na ugonjwa huo kuambukiza kwa kugusana.na.hali ya hewa.

Gazeti hili limepata kuwahoji baadhi ya wananchi ambao wengi wamesema walikuwa bado hawana taarifa hizo hivyo imetokea kwao kwa kushtukiza Ila elimu zaidi inahitajika kutolewa kwao.

Tunangojea taarifa zaidi kutoka kwa uongozi wa mkoa baaada ya kikao Chao Cha kujadili suala hilo la udhibiti wa ugonjwa huo ambapo kwa nyakati tofauti mkuu wa mkoa wa Arusha amesema Serikali imejipanga kudhibiti ugonjwa huo.

No comments:

Post a comment