Na John Walter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amewataka vijana wajiunge katika vikundi ili waweze kupata mikopo inayotolewa na serikali kupitia Halmashauri za wilaya na miji.
Gekul ameyasema hayo wakati akizungumza na Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi wa kata ya Bagara mjini Babati, wakiwa kwenye kikao cha ndani kilichofanyika hivi karibuni katika ofisi za kata hiyo.
Hango Shabani Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Bagara, amekiomba chama hicho pamoja na serikali kuwawezesha vijana na kuyafanyia kazi maombi yao ya fursa walizoziomba  kupatiwa katika Halmashauri ya mji wa Babati.
Mwenyekiti huyo amezitaja fursa walizoomba ni pamoja na ukusanyaji wa taka ndani ya mji wa Babati,kukusanya ushuru wa maegesho ya magari na kuwasaidia vijana kupata mikopo inayotolewa na serikali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul na Diwani wa Kata ya Bagara Nicodemus Bonifasi wameahidi kuyafanyia kazi maombi yaliyotolewa na vijana hao.
Mbunge huyo alimwakilisha Mwenyekiti wa jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Manyara, Ndugu, Mosses Komba.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: