Profesa Lazaro Busagala,Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya nchini (TAEC) akizungumza na washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa usalama wa mionzi yaliyofanyika Makao makuu ya Tume hiyo Jijini Arusha.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ya siku tano kutoka Serengeti Breweries mafunzo ya usimamizi wa usalama wa mionzi yaliyofanyika Makao makuu ya Tume hiyo Jijini Arusha.

 Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya  mafunzo ya usimamizi wa usalama wa mionzi yaliyofanyika Makao makuu ya Tume hiyo Jijini Arusha.  Mgodi  wa Bulyahulu
 Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TAEC Dkt.Justine Ngaile akitoa kutoa elimu kuhusiana na mionzi madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mionzi 

Mafunzo yakiendelea juu ya kuhusiana na mionzi madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mionzi

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TAEC Dkt.Justine Ngaile akiwa katika picha ya pamoja siku ya ufunguzi rasmi ya mafunzo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo


Na.Vero Ignatus,Arusha

Imeeelezwa kuwa Teknolojia ya Nyulia na mionzi kwa ujumla ina faida kubwa katika kuongeza uchumi wa Taifa ikitumiwa vizuri na siyo kwamba ina madhara katika afya ya binadamu pekee kama vile watu wengi wanavyofahamu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala kwamba teknolojia hiyo imeweza kutumika kwenye kilimo,Afya,kuhifadhi vyakula,viwandani hivyo ni vyema jamii itambue kuwa teknolojia karibia zote hapa duniani zina faida na hasara zake.


''Teknolojia ya Nyuklia na mionzi haina hasara bali ina faida kubwa kwani Teknolojia hiyo ya nyuklia  imeweza kuleta mbegu bora zaidi za mpunga ambayo imetoka mwaka 2019''

Amesema Teknolojia hiyo ya mionzi  inaweza kuwapa Watanzania chakula kilicho salama zaidi  kwasababu mionzi haibaki kwenye chakula ni tofauti na kuweka kemikali kwaajili ya  kuhifadhia vyakula

"Hii ni sawasawa na piga tochi ukizima tochi ule mwanga haubaki kwenye chakula hivyo ni salama zaidi kuliko ambavyo unaweza ukachukua kemikali ukapitisha kwenye kiwanda ukahifadhi vyakula hivyo

Profesa Busagala  alisema kuwa TAEC itaendelea kuboresha maeneo ambayo yanaonekana yanahitai maboresho zaidi sambamba na kutoa ratiba ya mwaka ambapo tayari imekwisha kuanza mwaka huu 2020 na kuboresha namna ya kuwasikiana na Taasisi mbalimbali  

Akifunga mafunzo ya yaliyoendeshwa kwa siku 5 juu ya usimamizi wa usalama wa mionzi kwa wafanyakazi wanaotumia vifaa vitumiavyo mionzi migodini viwandani na kwa watengenezaji wa vifaa vya mionzi vya hospitalini,waitumie elimu hiyo kwa manufaa ya jamii inayowazunguka

Awali akifungua mafunzo hayo juzi feb 18 Kaimu mkurugenzi mkuu wa TAEC Dkt.Justine Ngaile alisema lengo kuu ni kutoa elimu kuhusiana na mionzi madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mionzi.

Alisema kuwa sheria inayosimamia udhibiti wa matumizi salama ya mionzi namna bora ya kujikinga dhidi ya madhara ya mionzi(Radiation protection Principals )kwa kuzingatia kanuni za ulinzi wa mionzi katika kuhakikisha usalama wa watumiaji wa watengenezaji wa mashine za Midaki (X-Ray Baggage Scanner)

Dkt.Ngaile alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kupata elimu juu ya matumizi salama ya vyanzo vya mionzi ili kujikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi katika maeneo yao ya kazi.

Aidha mafunzo hayo yaliweza kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 16 kutoka migodi ya Bulyahulu ,Kampuni ya soda ya Cocacola,Serengeti Breweries ,watengeneaji wa vifaa vya mionzi (Repair and Maintenance ofa Nuclear Equipments)Hospitali ya Bugando ,Oceanic Pacific na Archelis.

Sambamba na hayo Majukumu ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni pamoja na kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini,kuhamasisha na kupanua matumizi salama ya Teknolojia ya Nyuklia na kutoa ushauri na taarifa mbalimbali za Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia

Mwisho.




Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: