Friday, 14 February 2020

SAUTI YA BUSARA YATIKISA ZANZIBAR

Wasanii mbali mbali wakiwa katika maandamano ya Sauti ya Busara Zanzibar
Mambo ni moto siku ya maandamano ya siku ya Busara

(Picha zote kwa hisani ya Link Reuben, Sauti za Busara).

MAANDAMANO ya ufunguzi wa tamasha la 17 la Sauti za Busara (Carnival Parade) mchana wa Februari 13 limetia fora kwa vikundi zaidi ya 16 kuonyesha sanaa yao mitaani .Mwandishi Andrew Chale anaripoti kutoka Zanzibar

Paredi hilo la aina yake likiwa pamoja na wananchi mbalimbali lilitumia umbali wa kilometa 1.6 kutokea Mapinduzi Square  hadi viunga vya Ngome Kongwe, katika bustani ya Forodhani.

Aina ya sanaa walioonyesha ni pamoja na ngoma za asili, sarakasi, muzikisanaa ya kutembea na magongo (ngongoti) ambapo ilikuwa shamrashamra njia nzima ulimopita msafara huo.

Nae msimamizi wa Paredi hiyo akizungumza na wanahabari,  Kharid Mselemu amesema tamasha hilo kila mwaka linakuwa na shamrashamra ya paredi kutoa fursa kwa  wasanii wachanga kuonesha sanaa yao.

"Wasanii wanapata fursa kuonyesha sanaa zao kwa wakati mmoja.

Pia ndio sehemu ambayo wanauza sanaa yao nje ya mipaka yetu. Hivyo tunatoa fursa kwa vikundi vichanga na vile ambavyo vunapata nafasi basi tunajumuika navyo" alieleza Kharid Mselemu.

Mselemu ameongeza kuwa, katika vikundi hivyo 16 pia kulikuwa na kikundi cha watoto wadogo ambao ni wanafunzi waliokuwa wakicheza ngoma na mitindo mingine ya sanaa.

Mselemu alivitaja baadhi ya vikundi vilivyoshiriki tamasha hilo ni pamoja na :
The Dream,  Mwanandege, Mbwakacheka (Ben), Kingwendu, Cha'?-Uruguay.

Vingine kikundi cha Shule ya Mwemberadu,Ngongoti, Sesembuge, Mdumange, na  vingine vingi.

No comments:

Post a comment